Sunday, 30 August 2015

KESI YA TALAKA YA MMILIKI WA ST. MATHEW YAAHIRISHWA TENA



Na Mwandishi wetu

MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala, Dar es Salaam, imepanga Septemba Mosi mwaka huu kutoa hukumu katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali zenye thamani ya Sh Milioni 800 inayomkabili Mmiliki wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks, Thadei Mtembei.

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa juzi lakini iliahirishwa kutokana na upande wa mlalamikaji kutofika mahakamani.

CHADEMA YAZINDUA KAMPENI JIMBO LA KALENGA






Na Mathias Canal, Iringa 
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa katiba ya Wananchi {UKAWA} kimezindua kampeni zake katika Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa kwa muktadha wa kuanza vyema mikikimikiki ya kumnadi mgombea wake ambaye mara kadhaa amesikika akisema jimbo hilo limekosa muwakilishi wa wananchi bungeni. 

Chadema/ukawa inataraji kuanza kampeni zake za kumnadi mgombea wa Urais, wagombea ubunge, na udiwani mara baada ya uzinduzi wa kampeni zinazotaraji kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo zilizofanyika katika eneo la Ifunda, mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema/Ukawa, Mdede Mussa Leonard amesema kuwa ameamua kugombea jimbo hilo kwa kuwa ni mkazi wa Kalenga hivyo hakusoma kwenye kitabu changamoto za jimbo na wala hana haja ya kusimuliwa.

Thursday, 27 August 2015

SERIKALI KUZINGATIA USHAURI WA RIPOTI YA ESRF YA MAENDELEO YA BINADAMU




Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) akimlaki Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha kufungua warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)



Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum ya mapumziko kabla ya kuingia katika ukumbi wa mikutano.



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifafanua jambo kuhusu warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na ESRF kwa mgeni rasmi (aliyeipa mgongo kamera) na meza kuu kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.

SANAA FASHION SHOW KUFANYIKA KESHO NDANI YA UKUMBI WA MBEZI GARDEN HOTEL




Na Andrew Chale, modewjiblog

(Dar es Salaam)-Ile shoo kubwa yamaonyesho ya mavazi ubunifu ya Tanzania katika kuibua vipaji vya wanamitindo chipukizi na models lililoandaliwa na kampuni ya Crown River Fame likijulikana kama Sanaa Fashion Show, linatarajia kufanyika Ijumaa hii ya Agosti 28, ndani ya ukumbi wa Mbezi Garden Hotel, ambapo pia kutakuwa na shoo kabambe kutoka kwa msanii wa THT, Msami.

Akizungumza na mtandao huu Meneja Mradi wa Crown River Fame, Mr. Rahul anasema tayari taratibu zote zimeshakamilika na models pamoja na wabunifu wa mitindo wameshakamilisha kazi zao na kinachosubiriwa na shoo hiyo kabambe na ya aina yake kwa upande wa fashion show.

"Tunataraji kuwa na Models zaidi ya 20, watakaonyesha mavazi ya ubunifu katika shoo hii ya Sanaa Fashion, na pia tunatarajia kuwa na wabunifu zaidi ya 15 wakiwemo wakongwe na wanaochipukia kwa maana 'Upcoming Desgners'.

Ili kuleta mageuzi katika tasnia hii ya urembo na ubunifu, jukwaa hili la Sanaa Fashion Show, lina lengo kuu la kuinua models wanaochipukia 'Upcoming models' na pia kuendeleza tamaduni zetu kwa maana hiyo tumeipa jina la Sanaa.".

Aidha, anabainisha kuwa, baadhi ya wabunifu wa mavazi watakaoshiriki kwenye kuvisha Models, katika show hiyo ni pamoja na Mama wa Mitindo nchini, Asia Idarous, Mohammed Abdul, Joyce na wengine wengi.

Kwa upande wa kiingilio ni V.I.M ni Sh 20,000 huku V.I.P yenyewe ikiwa ni sh 40,000.

Kwa upande wa wadhamini ni pamoja na MODEWJIBLOG, 8020Fashions, Shear Illusions, Mbezi Beach Garden, BR Production, MC na wengine wengi.

Husna Tandika akimfanyia make up, Model, Abdul-Amad katika duka la Shear Illusions Millenium Tower, jijini Dar es Salaam. Ikiwa tayari kwa maandalizi ya shoo hiyo ya kesho!



Jonetha-Peter. akipakwa make up na mfanyakzi wa Shear Illusions, Agnes Rafael..



Barnabas Lukindo akifanyiwa make up..



Calisah Abdulhameed akifanyiwa make up



Husna Tandika akimpaka Natasha Mohammed model make up

Wednesday, 26 August 2015

MISATAN to sharpen Bloggers & Editors’ skills on RTI, Election Reporting





By Gasirigwa GS

The Media Institute of Southern Africa (MISA) Tanzania Chapter in association with the Centre for ICT Policy promotion in Africa (CIPESA) will tomorrow train a selected number of bloggers and editors on Right to Information with special focus on this year’s general election.

Editors and bloggers will be taught on the safest ways to access information and report responsibly during campaigns and the entire election period. Attention will be directed to the Cyber crime and the Statistics Acts which are already in effect and have dire consequences on media practice. 

Participants will also be introduced to ‘The Broadcasting Services (Content) (The Political Party Elections Broadcasts) Code 2015’ which was gazetted on June 26, 2015.

Bloggers, SMS pollsters, and broadcasters in general will seriously be affected by this Code. The Code was developed by the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA).

About 20 selected Dar es Salaam-based editors and bloggers have confirmed to take part in this one-day workshop, scheduled for tomorrow Thursday the 27th of August at Kebbys Hotel in Dar es Salaam.

Similar training was held two weeks ago in Mwanza and drew participants from Geita, Mara and Mwanza itself. The Mwanza training specifically targeted journalists who basically cover rural areas.

MISATAN and CIPESA believe that the media needs to responsibly serve the public in a way that will provoke positive engagement and subsequent improvement in the political administration of the country.

HUKUMU YA MMLIKI WA ST. MATHEW YAAHIRISHWA HADI IJUMAA



Na Mwandishi wetu

MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, imeshindwa kutoa hukumu kwenye kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na mkazi wa Singida, Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks,Thadei Mtembei.

Katika madai yake ya Msingi, Mwangu anaomba mahakama imuamuru mdaiwa kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.

Hakimu wa mahakama hiyo Rajab Tamaambele akiahirisha alisema kwamba mzee mmoja wa mahakama amefiwa.

Mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu hiyo Ijumaa Oktoba 27.

Katika kesi hiyo Miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapo ni pamoja na Mwangu ambaye alidai kuwa alianza kuishi na Mutembei mwaka 1995 Kongowe Mbagala ambapo mwaka 1998 alikwenda kwa wazazi wa Mwangu kijiji cha Kwaye Iguguno Singida ambapo alitoa mahali na walifunga ndoa ya kimila. 

Alisema mtoto wa kwanza alizaliwa mwaka 1998, huku mtoto wa pili akizaliwa mwaka 2000 na mtoto wa tatu 2003

Katika ushahidi wao, watoto wa Mwangu ambao wanasoma katika shule za St Mary’s International na Hijra Seminari ya Dodoma, wamedai kuwa wanasumbuliwa ada na kwamba wanahitaji malezi yote kutoka kwa baba yao.

Watoto hao waliiambia mahakama kuwa, mara ya mwisho kumuona baba yao ni mwaka 2011.

Mtoto wa kwanza wa Mwangu alidai kuwa mwaka 2012 walifika katika Hoteli ya baba yao ya Sleep inn ndipo aliwafukuza na kuwaambia kuwa hawezi kuwalipia ada na badala yake aliwapa S.h 40,000 kila mmoja, fedha ambazo aliziacha mezani.

Pia walidai kuwa Mtembei aliwatolea maneno ya kashfa kwamba hata mama yao aende wapi, anao uwezo na kwamba anajeshi ambalo popote linafika.

Wakati wa ushahidi wake Mutembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.

Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye watoto watatu.


Monday, 24 August 2015

Wanafunzi waaswa kuzingatia elimu






Na Friday Simbaya, Iringa

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amewaasa wanafunzi wa kidato cha nne kuzingatia elimu na kusoma kwa bidii, kwa kuwa elimu ndiyo mkombozi wa maisha yao.



Rai hiyo aliitoa alipokuwa akitoa nasaha katika mahafali ya kidini kwa wanafunzi zaidi ya 50 wa umoja wa wakikristo wa wanafunzi Tanzania (UKWATA) yaliyofanyika jana katika Kanisa la KKKT Usharika wa Nyamhanga mjini Iringa.

Ibada maalum ya kuwaombea wanafunzi hao kutoka shule za sekondari za Efatha, Ipogolo, Tagamenda na Cagrielo katika Manispaa ya Iringa iliongozwa na Mchungaji Nuru Makweta kwa kushirikiana na Mchungaji Yekonia Koko ambaye pia mlezi wa UKWATA mkoa wa Iringa.

Mgeni rasmi Jesca Msambatavangu aliwataka wanafunzi hao wanapopata fursa ya kusoma waoneshe bidii darasani ili wajikomboe ili kutimiza malengo yao ya baadaye.

“Lazima muwe na maono ya mbali yakutaka kuwa kina nani hapo baadaye katika taifa hili,”alisisitiza Msambatavangu.

Mbali na kujikomboa, Msambatavangu alisema juhudi katika masomo yao zitasaidia kujiwekea misingi imara wa kujitegemea hapo baadae.

Katika hafla hiyo, mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Iringa wamekabidhiwa wanafunzi misaada shilingi laki nane pamoja vyeti vya uanacha wa UKWATA. 

Aliwaasa wanafunzi wa kidato cha nne shule za sekondari za Efatha, Ipogolo, Tagamenda na Cagrielo ambao wapo kwenye umoja huo (UKWATA) kusoma kwa bidii ili kukabiliana na changamoto za maisha hapo baadaye.

Msambatavangu alikuwa alikuwa akiwapongeza kabla ya kuanza kwa mitihani yao hapo tarehe 02.11.2015.



MSINDAI KUGOMBEA UBUNGE SINGIDA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA



Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida na Mwenyekiti wa wenyeviti CCM mikoa ya Tanzania, Mgana Izumbe Msindai, akikabidhiwa fomu na msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya manispaa ya Singida, Joseph Mchina ya kugombea ubunge jimbo la Singida mjini kupitia tiketi ya Chadema.

LOWASSA NDANI YA DALADALA

Mgombea Urais wa Chadema kupitia UKAWA, Edward Lowassa akiwa kwenye daladala asubuhi hii kuangalia kero za wananchi maeneo ya Gongo la mboto kuelekea Chanika.

UN KUBORESHA VYOO VYA SHULE 10 KILIMANJARO



Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Kiboriloni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kuweka msingi kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo. Kulia kwake ni Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu, Moshi

MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa nchini, yatasaidia kuboresha vyoo katika shule 10 zilizopo katika manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.

Hayo yalisemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya choo katika shule ya msingi Kiboriloni.

Alisema pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka watoto kukumbuka kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...