Tuesday, 5 January 2016

MAGAZETINI LEO JUMATANO


WANASIASA WAKWAMISHA SHUGHULI ZA URAGHABISHI WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI



Mchungaji wa kanisa la Umoja wa Makanisa ya Ubatizo Lucas Machibya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu baadhi ya shughuli za uraghabishi katika kijiji cha Pandagichiza 



Na Krantz Mwantepele ,Shinyanga 

Si mara nyingi viongozi wa kidini hujihusisha moja kwa moja na harakati za kisiasa ila wamekuwa mstari wa mbele kukemea matendo yanayofanywa na wanasiasa. Hawafanyi hivyo kwa bahati mbaya ila kutokana na nafasi yao katika jamii, hususani kuwaongoza waumini wao kwenda mbinguni. 

Hata hivyo, hii haimaanishi hakuna kabisa viongozi wa dini waioamua kujiingiza katika harakati za siasa ili kuleta maendeleo ya watu kwa haraka na ufanisi. Mchungaji Lucas Machibya ni mmoja kati ya viongozi wachache wa dini wanaoingia katika siasa. 

Huyu ni mchungaji wa kanisa la Umoja wa Makanisa ya Ubatizo lililopo katika kijiji cha Pandagichiza chenye wakazi wanaokadiriwa 2,481, idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake wanaokadiriwa kufikia 1,476. Hiki ni moja ya vijiji vilivyopo wilaya ya Shinyanga Vijijini, jimbo la Solwa.

Machibya ni mmoja wa wachungaji waraghbishi toka mkoa wa Shinyanga ambao uraghbishi wao umepelekea wananchi kumchagua kuwa mwenyekiti wa kijiji. Kujibainisha kwake kama mtu mwenye uwezo wa kusimamia anachokiamini na kushawishi wananchi kutambua majukumu na haki zao na jinsi ya kuzidai vimekuwa nguzo yake kubwa ya kukubalika. 

Kama walivyo wananchi wengi wa kijiji chake, yeye ni mkulima mdogo ambaye pia ni mwanachama wa Mtandao wa Wakulima Wadogo Tanzania (MVIWATA). Kupitia mwaliko wa mkulima mwenzake, Elizabeth Edward, Machibya amefanikiwa kupata maarifa ya uraghbishi na jinsi ya kufanya uraghbishi; uwezo wa kuwashawishi na kuwahusisha ama kuwachokoza watu ili waweze kujitambua na kutojiona wao ni wa jamii ya chini. 

Sifa iliyomfanya aalikwe kwenye mafunzo ya uraghbishi ni uwezo wake wa kuhoji mambo mbalimbali pasipo kukata tamaa kama anavyosema mwenyewe:

“Mimi ni mtu wa kuhoji vitu na si mtu wa kuridhika ama kukaa kimya n’napoona kuna jambo sijalielewa. Kwa kweli yale mafunzo yalinifanya kujiona mtu tofauti sana nikijilinganisha na nilivyokuwa awali. Nilijihisi tayari nimekuwa mtaalamu wa masuala ya uwajibikaji na utawala
bora.”

Kwa kuwa wao ni wakulima, walianza uraghbishi wao kwa kutaka kujua nini kinaendelea kuhusu bei ya pamba. mchungaji Machibya anaeleza ilivyokuwa:

“Kule tulifundishwa jinsi ya kuuliza maswali. Na cha kwanza tulichotaka kujua ni kwa nini bei ya zao letu la pamba imeshuka sana. Hili tuliliuliza sisi sote, mimi na waraghbishi wengine.”

Hawakuishia hapo tu bali wakaanza pia kufuatilia mapato na matumizi ya fedha za kijiji toka kwa viongozi wao. Walifanya hivyo kwa kuwatembelea ofisini na kuomba kupatiwa taarifa hizo na pia walitaka kufanyika mikutano ya hadhara. Baada ya harakati hizo kushika kasi, iliwabidi waongeze watu wengine zaidi kwa kuwatembelea majumbani kwao na kuwaraghbisha.

“Mchungaji aliomba kunitembelea nyumbani na alipofika alinipatia elimu. Kimsingi, alitaka nijitambue kwa kujua wajibu na haki zangu. Alinitaka nisiogope kuuliza maswali kwenye mikutano kwa
kuwa tuna uhuru wa kufanya hivyo. Nikajua kuwa nina wajibu kuuliza na kujua mapato ya fedha za kijiji na na matumizi yake kuwa hiyo ni haki yangu,” anaeleza Bw. Daudi
Denis toka kijiji cha Pandagichiza.



Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Pandagichiza wakiwa na waandishi wa habari za mtandaoni katika moja ya jengo la jiko la shule ya msingi Pandagichiza ambalo limetoakana na juhudi zao za uraghabishi 


Kufanikisha haya yote kumewajengea uaminifu mkubwa sana waraghbishi na baadhi yao wamekuwa wakishirikishwa katika
vikao muhimu vya maendeleo na serikali yao ya kijiji. Baadhi yao wametokea kuaminika zaidi na jamii kiasi cha kuombwa wagombee nyadhifa mbalimbali za uongozi wa serikali na ndani ya vyama vya siasa kama ilivyokuwa kwa mchungaji
Machibya.

Monday, 4 January 2016

Pam D Ft Mesen Selekta – Popo lipopo (Official Video)




LINK YA YOUTUBE: https://www.youtube.com/watch?v=MYgsBRcpi1c

WATANZANIA MSIKUBALI KUTOZWA RUSHWA KWA AJILI YA DAMU - DK. KIGANGWALLA



Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo watamchukulia hatua kali.

Kauli hiyo imetolewa mapema jana na Naibu huyo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.

Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.

“Kwa watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!. Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.

Mtu atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja, hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.

Awali katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.

“Motisha sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu..

Lakini kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.

“Mnatakiwa muwe na mfumo wa kumpa taarifa pindi damu yake imetumika, ikiwemo kumueleza kuwa damu yako imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua na kutokwa damu nyingi, na mtu huyo akipata taarifa hiyo ni motisha tosha hivyo ni lazima muwe na huo mfumo kutoa motisha zaidi.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla na msafara wake wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara mbalimbali katika ofisi hizo, Januari 4, 2016

Awali akielezwa na Meneja wa kanda ya Mashariki katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo, Kwa hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmshauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha ilikusapoti mpango wa damu salama.

Katika hilo Dk. Kigwangalla ameapa kuwashughulikia wale wote watakaozembea na kuwachukulia hatua kali Ma DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka zilizopo na kufukuzwa kazi.

“Naziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa ukusanyaji damu salama. Na Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na Mkurugenzi wake tutahakikisha tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili uteuzi wao ukome mara moja. Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito wapoteze damu wakati wa kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha kwa sababu ya watu hawataki kutimiza wajibu wao.

Hilo haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali ya damu kwa Tanzania kwa sasa unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha chini mno, tokea wafadhili wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini sana maana leo mzima kesho umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja damu nyingi zimemwagika unahitaji damu!!

Kwa upande wa watu wote wanaopata damu salama nchini, huduma hiyo wanazipata bure kwani damu hizo ni za Serikali, Hata hivyo mifuko na vitu vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo vina gharama kubwa.

“Damu inatolewa bure na serikali. Mtambue kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii ni gharama kubwa. Hivyo mifuko mashirika ya Bima, na mashirika mengine kuanzia leo kutazama namna ya kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu hizo. Damu ni bure, lakini mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama kubwa sana na hata vifaa vya kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa hivyo walipie kwa kila damu watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.


Meneja wa kanda ya Mashariki Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu wa ukusanyaji wa damu unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla (aliyeipa mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu wanaofikia kuchangia damu kwa hiari na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016 katika ofisi hizo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akitoa mkono wa pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo kwa kufika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4, 2016 na kuchangia damu kwa hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii ni mara yake ya nne na ni utararibu aliojiwekea.



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisalimiana na kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake halikuweza kupatikana) aliyefika kuchangia damu kwa hiari, Januari 4, 2016 katika makao makuu ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini Dar es Salaam.


Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.


Mmoja wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisaini vitabu vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kuzungikia vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam.


MAGAZETIINI LEO JUMANNE







































IRINGA MUNCIPAL COUNCIL VOWS TO INCREASE REVENUE COLLECTION





IRINGA Municipal Council (IMC) plans to raise the revenue collection from 2.5 billion shillings to reach seven billion shillings during the 2016/2017 financial year in order to improve and provide key social services for people, hence economic development.

Iringa Urban Municipal Mayor Alex Kimbe made the statement in his New Year message when he was addressing a public meeting organized by Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) meant to thank Iringa residents for voting them into power in which they won the parliamentary seat and 14 seats for ward councilors.

The mayor who is ward councilor for Isakalilo Ward (CHADEMA) in his new year message during public rally held at Mwembetogwa grounds said he thanked the Iringa urban residents for trusting them by giving them a landslide victory during the October 25, 2015 general elections in which the won a parliamentary seat and 14 out 18 wards. 

Iringa urban Constituency Member of Parliament Rev. Peter Msigwa (CHADEMA) said together with the full council members in collaboration council experts they have planned to improve the town council to become a city in the near future and urged the municipal authority to survey as many plots as possible so that they can avoid squatter houses.

Rev. Msigwa said the problem of squatting in Iringa town is due to lack of demarcated plots which forced people build houses in unlawful areas which later on demolished by the government for not following the procedures of town council by-laws.

He said there should be no urban farming to be conducted within the municipal council area but such farming practice should be done outside the urban area.

He said that there some people with financial power possessing large areas of land in town and was practicing commercial farming instead doing such kind of farming outside the urban center, adding that all those people with bigger lands, their lands should be re-demarcated and give land to people who don’t have land.

During the meeting, attended also by special seats members of parliament Suzan Mgonokulima (CHADEMA) and Grace Tendega (CHADEMA), Mayor of the Municipality of Iringa Alex Kimbe and all councilors of the party, Rev. Msigwa said apart from the traders, the municipal council councilors will cross-check with the statements of payment taxes, especially the buildings of Chama cha Mapinduzi (CCM) in Iringa which he claimed that they were tax invaders.

"There are allegations that puts CCM here Iringa not paying taxes on his various buildings. These buildings including Samora memorial stadium, CCM Regional office building and also some business stalls popularly known as ‘Vibanda vya CCM’, "Rev. Msigwa said.

MP Msigwa said they will do the verification in all these buildings to make sure there is legitimacy of the government which enables them to collect taxes from various projects paid the required taxes.

On her part, CHADEMA Regional Party Secretary Suzan Mgonokulima has asked Iringa residents not to doubt their performance of elected opposition party leaders but should trust them they will undertake the development that was true for the municipality and his people.


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...