Wednesday, 10 May 2017

ZIMWI LA AJALI LAZIDI KULITESA TAIFA




Basi la Ally's lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora limegongana na Coaster ya Isanzu uso kwa uso iliyokuwa linaelekea Mwanza kutoka Kahama


Ajali imetokea saa mbili asubuhi eneo la Samuye barabara ya Shinyanga.Hali ya dereva wa Coaster ya Isanzu si nzuri.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Muliro Jumanne amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni ya Ally's kuwa kwenye mwendo kasi.

Jumanne amesema kuwa abiria waliokuwa kwenye magari hayo ni zaidi ya 70 lakini waliojeruhiwa ni 35 ambao ndiyo wamelazwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk Rashid Mfaume amesema amepokea majeruhi 35 wa ajali hiyo wakiwemo watoto wawili na kwamba kati ya majeruhi hao wenye hali mbaya ni wawili.

BUNGE LATHIBITISHA KUPATA MAJINA KUWANIA UBUNGE EALA KUTOKA CHADEMA



1.Tarehe 4 Aprili, 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya Uchaguzi wa kuwachagua Wajumbe Tisa (9) wa Bunge la Afrika Mashariki watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo. Katika Uchaguzi huo, Wajumbe Sita (6) kutoka Chama cha Mapinduzi na Mjumbe mmoja (1) kutoka Chama cha Wananchi (CUF) walichaguliwa. Wagombea wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)walikosa kura za kutosha kuwapatia ushindi.

2.Hivyo, Bunge linapaswa kufanya uchaguzi kwa mara ya pili ili kuwapata wawakilishi Wawili (2) kutoka katika Kundi la Vyama vya Upinzani ambapo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho chenye hakiya kujaza nafasihizo.


3.Katika mazingira hayo na kwa kuzingatia masharti ya Sheria na Kanuni zinazotawala Uchaguzi huo, na kwa mamlaka niliyonayo kama Msimamizi wa Uchaguzi nilitoa TAARIFA ya Siku ya Uteuzi na Siku ya Uchaguzi kwenye Gazeti la Serikali Na. 537 la tarehe 21Aprili,2017. Taarifa hiyo ilitaja Sikuya Uteuzi(nominationday) wa Wagombea kuwa ni tarehe 03 Mei, 2017 Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni na Siku ya Uchaguzi(electionday) kuwa nitarehe 10 Mei, 2017.


Hata hivyo, tarehe 28 Aprili, 2017 Chama cha CHADEMA kiliandikia barua na kuiwasilisha kwangu siku ya tarehe 2 Mei, 2017 Jioni. Barua hiyo ilitoa maelezo kwamba muda waliopewa kuwasilisha majina ya wagombea kupitia kwenye Taarifa hiyo ni finyu kutokana na kuathiriwa na kuwepo kwa siku za mapumziko ya mwisho wa wiki pamoja na Sikukuu ya Mei Mosi iliyoanguakia siku ya Jumatatu hivyo, kuwepo kwa ugumu wa kufanya vikao vyao.


5.Kutokana na sababu hiyo, Chama hicho kiliomba kuongezewa muda usiopungua wiki mbili ili kiweze kukamilisha mchakato wa uteuzi wa wagombea, kupata uthibitisho wa uraia kutoka Idara ya Uhamiaji na uthibitisho wa sifa za kugombea kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 50 (2) ya Mkataba ikisomwa pamoja na Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania,1977.


6.Kutokana na sababu zilizotolewa, niliongeza muda wa siku 4 kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 7 Mei, 2017 ili kukiwezesha Chama hicho kukamilisha taratibu hizo za kisheria na hivyo kukitaka kuwasilisha kwangu majina na nyaraka za wagombea waliowateua tarehe 8 Mei, 2017 kabla ya Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni ambayo ni Siku ya Uteuzi wa Wagombea(nomination day).


7.Kupitia taarifa hii, napenda kuujulisha umma kwamba Chama cha CHADEMA kimewasilisha kwangu majina sita (6) ya Wagombea wa nafasi mbili za ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki. Kati ya wagombea hao wanne (4) ni wanaume na wagombea wawili (2) ni wanawake.Majina hayo yamewasilishwa kwangu jana tarehe 8 Mei, 2017 kabla ya mudawaSaa 10 Jionikama nilivyokuwa nimeelekeza.


8.Baada ya hatua hiyo,nilifanya uchambuzi wa Nyaraka zilizowasilishwa ili kujiridhisha na uzingatiwaji wa masharti ya uteuzi wa Wagombea kwa mujibu Ibara ya 50 (2) ya Mkataba, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Kifungu cha 4 (4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki na Kanuni 5 (2),(3) na Kanuni ya 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge,ToleolaJanuari,2016.


Matokeo ya uzingatiwaji wa masharti hayo yameainishwa katika Jedwali lifuatalo:
TANBIHI:


√-Maana yake sharti husika limetimizwa


10.Uchambuzi huo umebainisha kuwa Wagombea wote wamekidhi vigezo na masharti yanayotakiwa kwa mujibu wa Sheria. Hivyo, napenda kutoa TAARIFA na KUWATANGAZA wafuatao kuwa Wagombea katika Uchaguzi wa Wajumbe Wawili (2) kupitia Kundi la Vyama vya Upinzani kutoka Chama cha CHADEMA uliopangwa kufanyika tarehe10 Mei,2017:

Tuesday, 9 May 2017

Mbunge wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wakabidhi Vifaa Kwa Shughuli za Kijamii




Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza nas Wananchi wa Shehia tatu za Bungi, Ubago na Tunguu wakati wa kukabidhi vifaa kwa ajili ya shehia hizo tatu kwa matumizi ya Kijamii wakati wa shida na raha, Vifaa walivyokabidi majiko ya gesi 3, sinia 800 mitungi ya gesi 6 na mabusati. kwa ajili ya matumizi yao katika shughuli za kijamii, hafla hiyo ya makabidhiani imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Wilaya ya Kati Unguja. Na kuhudhuriwa na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja. 



Mbunge wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Khalifa Salim Suleiman akizungumza na wananchi wa jimbo lake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii katika jimbo lao ikiwa ni kutimiza ahadi kwa wananchi wa jimbo lao walioitowa wakati wa kampeni ya uchaguzi.hafla hiyo imefanyika katika tawi la CCMTunguu Wilaya ya Kati Unguja.



Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi vifaa mbalimbali waliohidi kwa wananchi wa jimbo lao wakikabidhi vifaa hivyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdallah na Uongozi wa jimbo hilo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Tawi la CCM Tunguu Unguja. wakikabidhi mabusati na sinia.



Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakikabidhi majiko ya gesi kwa ajili ya shia tatu kila shehia imepata jiko moja na mitungi ya gesi miwili. na sinia 200, kwa ajili ya matumizi ya kijamii katika shehia zao.Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Unguja. 



Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi sufuria kwa Uongozi wa Jimbo kwa ajili ya matumizi ya Shehia za Jimbo hilo tatu kila shehia imepata sufuria mbili kubwa.


Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi mitungi ya gesi kwa Uongozi wa Jimbo kwa ajili ya matumizi ya Shehia za Jimbo hilo tatu kila shehia imepata mitungi miwili ya gesi mikubwa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii katika jimbo lao zilizotolewa na viongozi hao..



Mwenyekiti wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mzee Khatib Ramadhani akitowa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge kwa msaada wao huo kwa ajili ya kuwajali wananchi wa jimbo lao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia kwa malengo yaliokusudiwa katika shughuli za kijamii katika shehia husika za jimbo hilo. 



Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali dhamira wa msaada huo kwa wananchi wa jimbo lao kuweza kuwasaidia katika matumizi yao ya shughuli za kijamii zinazotokea kwa wananchi hao ili kuweza kuvitumia kupunguza gharama za kukodi vifaa hivyo.

MAGAZETI LEO JUMATANO




MAGAZETI KWA HISANI QUEEN ESTER TOWER HOTEL, KWA HUDUMA BORA KABISA!




























Monday, 8 May 2017

ANSGAR CUP 2017 PERAMIHO, NGOMA 'INOGILE'





Na Alex Mapunda, Ruvuma

MWAKILISHI wa Kata ya Peramiho katika Mashindano ya Ansgar Cup ngazi ya Tarafa, timu ya Afya Fc imefanikiwa kuitandika bila huruma Kilagano Fc timu toka Kata ya Kilagano kwa kichapo cha bao 3-0.


Katika mchezo huo ambao Mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Simon Bulenganija, bao la kwanza la Afya Fc liliwekwa kimiani na mshambuliaji machachari Emanuel Kajana dakika ya 39 ambalo liliwachanganya wachezaji wa Kilagano FC na wakaanza kucheza kwa Tahadhari kubwa.

Dakika 15 za kipindi cha pili Kilagano Fc walicheza vizuri mno na walifanikiwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la Afya Fc, lakini mambo yalikuwa tofauti baada ya mchezaji wa Afya Fc Shabiru Kinunga kuipatia timu yake hiyo bao la pili lililopeleka majonzi kwa Kilagano Fc mnamo dakika ya 60 ya mchezo.

Lakini Kabla ya mpira kumalizika mfungaji wa bao la kwanza Emanuel Kajana alishindilia msumari wa moto katika vidonda vya Kilagano Fc kwa kuipati Afya Fc bao la tatu kwa njia ya kichwa kunako dakika 88, bao ambalo lilikamilisha ushindi mnono wa bao 3-0 baada ya mwamuzi wa mpambao huo kupuliza filimbi ya mwisho kuashiria kwamba pambano limemalizika.

Katika mchezo wa mapema uliopigwa mishale ya saa nane mchana timu toka Kata ya Parangu ilikumbana na kipigo cha jumla ya bao 2-1 toka kwa Litisha Fc toka kata ya Litisha.

Kata zilizojitosa katika mashindano hayo ni Kata ya Peramiho, Litisha, Parangu, Kilagano, Lilambo, Maposeni, Mpandangindo pamoja na Liganga ambapo mechi za ufunguzi ilikuwa ni kati ya Litisha dhidi ya Parangu mishale ya saa nane mchana kisha saa kumi jioni Kilagano Fc wakakumbana na Peramiho (Afya Fc) kwenye uwanja wa Ansgar uliopo Peramiho B.

Mwaka huu zawadi zimeboreshwa toka shilingi 300,000/= kwa washindi wa kwanza hadi shilingi 400,000/= , 250,000/= washindi wa pili hadi shilingi 300,000 pamoja na 150,000/= washindi wa tatu hadi 200,000/= huku mchezaji bora akiambulia kifuta jasho cha shilingi 50,000/= hali ambayo imesababisha ongezeko la ushindani na kila timu shiriki inatamani kunyakua ubingwa wa mshindano hayo.

Ansgar cup ni moja ya ligi kongwe mkoani Ruvuma na imedumu kwa zaidi ya miaka 20, lengo kubwa la mashindano ya Ansgar yanayoandaliwa na mkurugenzi wa Hospitali ya Peramiho Dkt. Ansigar Stuffe OSB ni kuibua vipaji kwa wachezaji, burudani baada ya kazi, kuongeza soka la biashara kwa wafanyabiashara wa tarafa ya Peramiho n.k.

Baadhi ya wachezaji waliotokea Ansgar Cup ni pamoja ni Pato Ngonyani (MajiMaji na Yanga), Anold Nguruchi na wengineo wengi.

NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI




MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata mbalimbali mkoani hapa ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya afya kwa watoto (Toto Afya Kadi) ambapo uelewa wake umekuwa sio mzuri.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akizungumza na mtandao huu ofisini kwake ambapo alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa uelewa jamii kuhusiana na umuhimu na faida za huduma hiyo.


Alisema wakiwa huko watapita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni na kufanya mikutano ya nje kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa juu manufaa ya kuwaingiza watoto hao kwenye mfuko huo.

“Unajua hii huduma Toto Afya Kadi hasa kwa maeneo ya vijijini uelewa wake umekuwa sio mzuri hivyo sisi tumepanga kuanza kuhamasisha na kuipa uelewa jamii ili waweze kuitambua na kujiunga nayo “Alisema.

“Nia kubwa ni kutaka kuona jamii waliochini ya miaka 18 wana jiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani itawasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa sababu akishajiunga anaweza kupata matibabu bure “Alisema.

Sambamba na hilo alisema pia hivi sasa wanaihamasisha jamii kuendelea kujiunga nao ikiwemo wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.

“Lakini pia tunaendelea kuhamasisha wakina mama kujiunga na mradi wa KFW mradi ambao unaendelea kwenye mikoa ya Mbeya na Tanga kwani itawasaidia kupata matibabu pindi wanapokuwa wameugua “Alisema.

Akizungumzia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo,Meneja huyo alisema ni uelewa mdogo wa wananchi hasa maeneo ya vijijini na katakuchangamkia fursa za mfuko huo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha 


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...