Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof.
Idrissa Mshoro akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa
chuo hicho wa kuendelea na jitihada za kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka
na tanga ngumu ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya majaribio ya teknolojia za
kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani
kuwa mboji na gesi asili ya kupikia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa chuo
hicho Prof. Gabriel Kassenga
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa teknolojia za kibiolojia
zinazobadili tanga ngumu au maji taka (waste
treatment facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo
pichani) namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka inavyotumika
na kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo kupata mboji kwa
ajili ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya kupikia, ambapo mpaka sasa
kiasi cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na nyumba mia moja katika Chuo Kikuu cha Ardhi
zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa
Mshoro
Miundombinu ya majaribio ya teknolojia za
kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani
kuwa mboji zilizojengwa katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Ardhi, mtaa wa
Migombani, kata ya Segerea na katika kiwanda cha Madawa ya Binadamu cha Mansoor Daya Chemicals.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo na kutembelea maeneo
ilipojengwa miundombinu ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili taka ngumu au
maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji.
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwasha karatasi kwa kutumia Gesi
Asili iliyozalishwa na Mtambo huo. Picha
na Hassan Silayo-MAELEZO
No comments:
Post a Comment