Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (hayupo pichani) kufungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo.
Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalusesa wakati akifungua rasmi kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo. Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini.
Alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati akifungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.