Monday, 8 June 2015

USHAHIDI WAKWAMISHA KESI DHIDI YA UKATILI KWA ALBINO



Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari jamii na Mkufunzi Bi Rose Haji Mwalimu (aliyesimama) wakati wa ufunguzi kijiji cha Usagara, wilayani Misungwi mkoani Mwanza hivi karibuni.

Na Modewjiblog team, Mwanza

Tabia ya watu kukwepa kutoa ushahidi mahakamani ni sababu mojawapo ya wahalifu wa mauaji ya albino kutotiwa hatiani na kuachiwa huru.

Hayo yameelezwa katika warsha zilizoendeshwa mfululizo wilayani Misungwi, Kahama na Bariadi za ushirikishwaji wa jamii katika kuzuia na kutokomeza ukatili, unyanyasaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) nchini.

Wakichangia mada kuhusu changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi, washiriki wamesema kwamba imekuwa ni kawaida kwa watu kutokuwa tayari kutoa ushahidi mara wanapoitwa mahakamani kwa sababu zisizokuwa na mashiko.

Sababu hizo ni kuogopa kuuawa na wahusika na shinikizo kutoka kwa wanafamilia.

UJUMBE WA IRINA BOKOVA, MKURUGENZI MKUU WA UNESCO SIKU YA BAHARI DUNIANI



Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova.

DUNIA endelevu haiwezi kuwapo kama hakutakuwepo na bahari yenye kuendeleza uhai.

Miezi michache kabla ya kufanyika kwa kongamano la kihistoria la COP21 (21st Conference of the Parties to the United Nations Framework Convention on Climate Change) la kutengeneza ajenda mpya ya maendeleo endelevu, ujumbe huu ulikuwa hauna tija.

Lakini sasa ujumbe huu una tija sana na muhimu sana.

Iwe nchi iko mbali na bahari au karibu, kila nchi na kila aina ya uhai hutegemea zaidi namna bahari inavyokuwa salama na yenye kutekeleza wajibu wake wa kulea uhai.

Kiukweli bahari ni kitu muhimu katika mfumo wa hali ya hewa duniani, ikiratibu kwa namna ya kipekee mabadiliko ya muda mrefu ya hali ya hewa na mfupi na pia uwepo wa hewa mbalimbali katika anga ikiwemo oksijeni tunayovuta.

Aidha inawezesha kuwapo kwa lishe na kuwa chanzo cha chakula.

Wakati wanasayansi wanaweka teknolojia mpya kuweza kuangalia tabia za bahari , tunatambua kwamba zipo athari za shughuli za kibinadamu katika afya ya bahari hasa hewa ya ukaa inayozalishwa kwa sababu za shughuli za kiviwanda.

GREEN WASTE PRO LTD WASHINDI TUZO YA MAZINGIRA



Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena akitoa maelezo ya baadhi ya vifaa (havipo pichani) wanavyotumia katika kusafisha manispaa ya Ilala kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadiq akimkabidhi cheti na kikombe kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala, Hawa Sindo ambao wameibuka mshindi wa kwanza wa usafi wa mazingira mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe za kilele cha wiki ya mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Grace Mushi kutoka Green Waste Pro ltd.


Bi.Hawa Sindo (kushoto) akiwa na mfanyakazi mwenzake Grace Mushi ambao wote ni wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea tuzo ya mazingira.

JAPAN HANDS OVER MICHAKAINI 'A' PRIMARY SCHOOL BUILDING



The front view of the newly constructed Classroom block.






The rear view of the newly constructed Classroom block.




Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida posing with from left Chaiman of Parent Committee of Michakaini Primary School, Mr. Nassor HArith Mohammed, Hon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah - South Pemba Regional Commissioner, Headteacher Ms. Neema Mwalim Khamis, Secretary of the Committee and Head Teacher, in front of the newly constructed classroom block.






Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Prof. Ibrahim Lipumba, CUF Chairman, posing with Michakaini primary school pupils in front of the newly constructed classroom block.






Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Hon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah - South Pemba Regional Commissioner, during the Handing over ceremony.




Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Prof. Ibrahim Lipumba, CUF Chairman, during the Handing over ceremony.

Sunday, 7 June 2015

IHEFU MISITU FC YAINYUKA IHALIMBA VIJIJINI FC 3:2 LIGI YA UJIRANI MWEMA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmood Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini akifungua mashindano ya Ligi ya  Ujirani Mwema yalioandaliwa kwa udhamini wa Shamba la miti Sao Hill mjini Mafinga wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. walioketi kutoka kushoto ni Meneja wa Shamba la miti Sao Hill Salehe Beleko na Mwenyekiti wa CCM (W) Mufindi ambaye pia Diwani wa Kata ya MakunguYohanes Cosmas Kaguo.

Timu ya Ihefu Misiti FC ikipasha misuli kabla kuanza kwa mechi ya ufunguzi na Timu ya Ihalimba vijijini FC katika Uwanja wa Ihefu mjini Mafinga.



 Meneja wa Shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko (kushoto) akisalimia na golikipa wa Timu ya Ihalimba Vijijini FC kabla ya mechi kuanza.

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti Kamati ya Michezo Sao Hill Ligi ya Ujirani Mwema, Said Aboubakar, Meneja wa Shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko na Mwenyekiti wa CCM (W) Mufindi ambaye pia Diwani wa Kata ya Makungu, Yohanes Cosmas Kaguo pamoja wakifuatilia mechi katika Ihefu Misitu FC (wenyeji) dhidi Ihalimba, ambapo Ihefu FC iliibamiza Ihalimba 3-2 na goli zote zilifungwa kipindi cha pili cha mchezo. 

RAW MILK UNSAFE, CAUSES FOOD-BORNE DISEASES


TANZANIANS have been advised to drink pasteurized milk because it has higher levels of nutrients and other health benefits unlike raw milk.

Speaking on Friday during the press briefing, Asas Dairies Ltd, Events and Marketing Manager, Jimmy Kiwelu said drinking pasteurized milk (the process of heating milk for short time at high temperature) has a health nutrients contents.

KUTOKA KANISANI: TUSIWEKE HAZINA DUNIANI BALI MBINGUNI AMBAPO HAKUNA NONDO NA KUTU!


Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Mlandege mjini Iringa, Petro Majehe akihubiri injili ya Matheo 6: 19-21 katika ibada ya kwanza. Somo la leo lilikuwa wakristo wasiwekeze mali zao duniani ambapo kuna nondo na kutu pamoja na wezi bali wakeze hazina mbinguni ambapo hakuna nondo, kutu na wezi.

Alisema wanadamu wanapenda zaidi mambo ya duniani na kumsahau Mungu ndio maana kunamaovu mengi yanatendeka.
"Ilipo hazina zako ndipo moyo unakuwepo"

Friday, 5 June 2015

LOWASSA APATA MAPOKEZI MAKUBWA MKOANI MWANZA


Umati wa Wananchi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM waliojitokeza hii leo Jijini Mwanza kumlaki Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Mondule (CCM) Edward Ngoyai Lowassa. Lowassa aliwasili Mkoani Mwanza kusaka sahihi za wadhamini kwa ajili ya kupata fursa ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Umati wa Wananchi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza uliojitokeza Kumpokea Mbunge wa Jimbo la Monduli (CCM) na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa ambae baada ya Kutangaza nia ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kuchukua Fomu, ameanza harakati za kusaka sahihi za wadhamini ili kumwezesha kugombea nafasi hiyo.

MESSAGE FROM MS IRINA BOKOVA, DIRECTOR-GENERAL OF UNESCO, ON THE OCCASION OF WORLD ENVIRONMENT DAY



Director-General of UNESCO. Irina Bokova.

Seven Billion Dreams. One Planet. Consume with Care.

We live in a world transforming deeply, rocked by multiple crises, on a planet facing rising pressure.

Environmental change has never been so deeply interconnected with our societies as it is today, in this era that many scientists call the Anthropocene, when human activity is the major force shaping the planetary system. The impact that individual women and men are having on the sustainability of the planet may not always be visible -- but consider the impact of seven billion women and men, and it becomes clear that daily choices matter.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...