Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmood Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini akifungua mashindano ya Ligi ya Ujirani Mwema yalioandaliwa kwa udhamini wa Shamba la miti Sao Hill mjini Mafinga wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. walioketi kutoka kushoto ni Meneja wa Shamba la miti Sao Hill Salehe Beleko na Mwenyekiti wa CCM (W) Mufindi ambaye pia Diwani wa Kata ya MakunguYohanes Cosmas Kaguo.
Timu ya Ihefu Misiti FC ikipasha misuli kabla kuanza kwa mechi ya ufunguzi na Timu ya Ihalimba vijijini FC katika Uwanja wa Ihefu mjini Mafinga.
Meneja wa Shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko (kushoto) akisalimia na golikipa wa Timu ya Ihalimba Vijijini FC kabla ya mechi kuanza.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti Kamati ya Michezo Sao Hill Ligi ya Ujirani Mwema, Said Aboubakar, Meneja wa Shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko na Mwenyekiti wa CCM (W) Mufindi ambaye pia Diwani wa Kata ya Makungu, Yohanes Cosmas Kaguo pamoja wakifuatilia mechi katika Ihefu Misitu FC (wenyeji) dhidi Ihalimba, ambapo Ihefu FC iliibamiza Ihalimba 3-2 na goli zote zilifungwa kipindi cha pili cha mchezo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmood Mgimwa (kulia) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini akiwasili katika viwanja vya Ihefu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi ya Ujirani Mwema ya Sao Hill jana.
Mwenyekiti Kamati ya Michezo Sao Hill Ligi ya Ujirani Mwema, Said Aboubakar akisoma risala kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmood Mgimwa (kulia) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini
.
Hatari hatari katika lango la Ihalimba FC
mashabiki
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmood Mgimwa (kulia) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini akipiga mpira kuashilia uzinduzi wa Ligi ya ujirani mwema katika viwanja vya Ihefu mjini Mafinga jana.
Vikundi vya mazingira na Nyuki vikitumbwiza kwa pamoja wakati uzinduzi wa Ligi ya Ujirani Mwema Sao Hill.
No comments:
Post a Comment