Monday, 8 June 2015

GREEN WASTE PRO LTD WASHINDI TUZO YA MAZINGIRA



Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena akitoa maelezo ya baadhi ya vifaa (havipo pichani) wanavyotumia katika kusafisha manispaa ya Ilala kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadiq akimkabidhi cheti na kikombe kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala, Hawa Sindo ambao wameibuka mshindi wa kwanza wa usafi wa mazingira mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe za kilele cha wiki ya mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Grace Mushi kutoka Green Waste Pro ltd.


Bi.Hawa Sindo (kushoto) akiwa na mfanyakazi mwenzake Grace Mushi ambao wote ni wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea tuzo ya mazingira.


Msanii wa Bongo Movie nchini ambaye pia ni Balozi wa usafi na Mazingira wa Manispaa ya Ilala 2015/2016, Mohammed Mwikongi (wa tatu kushoto) akipozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala walioibuka kidedea mshindi wa kwanza wa usafi wa mazingira mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe za kilele cha wiki ya mazingira duniani zilizofanyika ndani ya viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.











Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa tuzo za mazingira kwa mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe za kilele cha wiki ya mazingira duniani zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...