Na Friday Simbaya, Iringa | | | ||
ASKARI polisi amefariki dunia baada ya kujipiga risasi mbili chini ya kidevu, kifo kinachosadikiwa kuwa kinahusiana na wivu wa kimapenzi baina yake na askari mwingine. Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla alisema askari huyo alijipiga na kufa papo hapo Julai 8, mwaka huu saa 3:00 usiku katika eneo la makazi ya mkuu wa mkoa wa Iringa eneo la Gangilonga, manispaa ya Iringa. Alimataja askari huyo kuwa ni G13 Mashauri (24) ambaye kabla ya kujiua alikuwa kwenye lindo eneo la benki ya CRDB ambako aliingia lindoni saa 12:00 jioni Julai 8, mwaka huu na kutoka saa 1:30 usiku kuelekea nyumbani kwa askari wa kike. Akielezea tukio Alisema baada ya kuachana kila mmoja aliendelea na mambo yake na hadi siku ya tukio Mangalla alisema askari huyo aliondoka kwenye lindo “Baada ya kufunguliwa alimkuta Zahara amekaa na kijana mmoja aitwae Sunday Tumaini mfanyakazi wa Bayport akawatishia, ndipo askari wa kike alipiga kelele kuomba msaada, askari mwingine aliyekuwa amepanga kwenye nyumba hiyo alitoka na kusaidia”alisema kamanda huyo. Alisema askari aliyekuja kumsaidia Zahara, alimnyang’anya silaha aliyekuwa nayo Mashauri na baada ya kunyang’anywa aliondoka eneo Alisema baada ya kuzungumza nao ghafla alimnyang’anya silaha askari mwenzake na kuondoka nayo kwenda kwenye eneo alilojiulia kwa kujipiga risasi mbili chini ya kidevu. Hata hivyo Mangalla alisema kuwa taarifa za awali za kujiua kwa askari huyo zinaonyesha alijiua kutokana na wivu wa kimapenzi lakini polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio | ||||
|
|
|
|
|
Saturday, 10 July 2010
ASKARI POLISI AJIUA KWA KUJIPGA RISASI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment