Saturday, 10 July 2010

MFUKO WA BIMA YA AFYA WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

Na Friday Simbaya,

Kilolo

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Iringa wametoa msaada wa magodoro 15, mashuka 20 na sabuni ya kufulia kwa Kituo cha Watoto ya Yatima cha Amani wilayani Kilolo Mkoa wa Iringa.

Mkurugenzi wa Mfuko Kanda ya Iringa Bi. Grace Lobulu amesema jana kuwa mfuko uliamua kuitumia siku hii sambamba na Wiki ya Bima ya Afya kufanya shuguli za kijamii ikiwemo kutembelea wenye maitaji na kuwafariji.

Amesema kuwa kwa kanda ya Iringa mwaka huu inasheherekea Wiki ya Bima ya Afya kwa kutembelea watoto yatima katika kituo Amani Center (wilayani Kilolo) kinachoendeshwa na Kanisa Katoliki Dayosisi ya Iringa ambacho kina watoto 86.

Mwaka huu wiki ya bima ya afya na ujumbe usemao, “Mtaji wa Mtanzania ni Afya Bora, Jiunge na NHIF/CHF Leo”

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Kituo cha Amani kaimu Meneja Bw. Wilfred Mwakalebela, aliushukuru mfuko huo kwa kuwapatia msaada wa pekee watoto huo na kuongeza kuwa ni mara ya kwanza kwa kituo hicho kupata msaada wa magodoro na mashuka tangu kuanshwa kwa kituo hicho.

Lakini pia mfuko utatembelea watoto waliopo katika Kituo cha watoto yatima cha Morogoro Orphanage center wilayani Songea vijijini mkoani Ruvuma amabacho kina watoto 120.

Katika kituo hicho cha Morogoro Orphanage Center, watoto yatima watapelekewa magodoro 20, mashuka 20, mabalanketi 20 na mafuta ya kupikia ndoo 10 (za lita 20).

Hata hivyo kuanzia mwaka 2007 Bodi ya Mfuko iliammua kuwa na wiki ya bima ya afya katika kipindi hicho cha maonyesho ya sabasaba na ambapo siku ya tarehe 30/06/2010 iliteuliwa siku maalum ya bima ya afya katika wiki hiyo.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...