Sunday, 11 July 2010

MWANAFUNZI WA MUCE AJITOSA KUWANIA UBUNGE MBINGA MASHIRIKI


Na Friday Simbaya,

Iringa

WANACHAMA zaidi wanatangaza nia kugombea ubunge katika majimbo kadhaa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tawi la Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa (MUCE), Nditi Edmund, ametangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Mbinga Mashariki mkoani Ruvuma.

Edmund ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Elimu cha Mkwawa, Mkoa Iringa, ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Mbinga Mashariki kupitia CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari jana chuoni hapo, Nditi Edmund alisema kuwa ameamua kugombea ili kuleta maendeleo na kudai kuwa jimbo hilo linakabiliwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja ukosefu wa miundombinu, soko la kahawa na elimu.

Alisema kuwa endapo akishinda atafanya mambo mengi kwa shirikiana na wananchi wa jimbo hilo pamoja na kushawishi serikali kujenga miundomibinu ya kilimo pamoja na kuwapatia wakulima soko la uhakika la kahawa ambalo kwa sasa sio nzuri sana.

Aliongeza kuwa Wilaya ya Mbinga iko nyuma katika sekta ya kilimo kutokana na ukosefu wa zana za kilimo pamoja na pembejeo.

Jimbo hilo la Mbinga Mashariki linalo shikiliwa na mbunge wa sasa Gaudence Kayombo wa CCM, mpaka sasa lina jumla ya watu waliotangaza nia ya kugombea kufikia tisa.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...