MGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mohamed Gharib Bilal ataanza ziara ya kampeni za uchaguzi kwa siku nne (4) mkoani Iringa, imeelezwa leo.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Mary Tesha, ilielezwa kuwa mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM ataanza ziara yake mkoani hapa tarehe 03-06/09/2010.
Katibu huyo wa mkoa amesema kuwa mgombea mwenza ataanzia Wilaya ya Ludewa ambapo atafanya mikutano mbalimabli katika maeneo ya Manda, Nsungu, Mkoma-ng’ombe, Ludewa mjini na kumalizia na Mlangali kabila yakuendelea ziara katika wilaya zingine mkoani hapa.
Wilaya hixo atakazozitembelea katika ziara yako ya kampeni ya uchaguzi ni pamoja na Njombe, Makete, Mufindi, kilolo na kumalizia na Iringa Mjini.
Aidha, Katibu huyo wa mkoa amesema akiwa Mjini Iringa Dkt. Bilal, atapewa taarifa fupi ya wilaya na baada ya hapo atahutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa kwenye mkutano utakaofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.
Hatamaye, mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, tarehe 06/09/2010 asubuhi ataagana na viongozi wa Mkoa wa Iringa katika Uwanja wa Ndege Nduli tayari kuelekea Mkoa wa Shinyanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment