Friday, 20 August 2010

MASHINDANO YA SHIMIWI 2010 KUFANYIKA TANGA

Mwandishi wa habari za michezo wa Nipashe kulia Bi. Bahati Moleli akifanya mahojiano na Kocha wa timu ya Ras Mkoa wa Iringa Bw. John Ndambalo (katikati) Ijumaa kuhusiana na mashindano ya wizara na serikali (SHIMIWI) 2010 na wa kwanza kushoto ni Mwandshi wa habari wa Mtanzania Bw. Onesemo Joseph (MIJO). Mashindano ya SHIMIWI yamepangwa kufanyika mkoani Tanga kuanzia Septemba 17 hadi Oktoba 2. Michezo itakayeshindanishwa ni soka, netiboli, riadha na kuvuta kamba. Kwa mjibu wa Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw.Ramadhani Sululu alisema, viwanja sita vitatumika kwenye michezo hiyo ambavyo ni Mkwakwani, Popatlati, Gymkhana, Disuza, Tanga School na Uwanja wa Bandari.Timu ya soka ya Ras wakijifua na mazoezi katika viwanja vya Mkwawa mjini Iringa.Timu ya Ras wakifanya mazoezi ya viungo jana.

No comments:

ASAS AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU VURUGU ZA UCHAGUZI

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas , amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchagu...