KAIMU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bw. John Mnyika, amempa siku 14 aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Isimani mkoani Iringa, Bw. Ben Kwapwani kutoa utetezi wake kwa maandishi kabla ya chama hicho hakitaja mwajibisha kwa kukikuka katiba ya Chadema.
Mbali na agizo hilo, pia Bw. Kapwani amesimamishwa rasmi nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa wa Chama hicho hadi hapo uongozi wa juu utakapojiridhisha kuhusiana na shutuma mbalimbali zinazomkabili kada huyo.
Kwa mujibu wa barua ya Mnyika ya Septemba 14 mwaka huu aliyomwandikia Kapwani, ikiwa na kumbukumbu namba C.HQ/ADM/M/IR/05 inaeleza kuwa miongoni mwa mambo anayotakiwa kutolea maelezo ni pamoja na kushindwa kurudisha fomu ya uteuzi ya kugombea ubunge katika Jimbo la Isimani.
Shutuma nyingine zinazotakiwa kutolewa maelezo ni kuonekana kwake machoni pa umma akimnadi mgombea wa chama kingine wakati Chadema imesimamisha mgombea wake wa ubunge Iringa mjini ambaye anakubalika na wananchi wengi.
Anadaiwa kumpigia debe hadharani mgombea ubunge wa NCCR-Mageuzi Mariam Mwakingwe ambaye pia anaungwa mkono na muungano wa vyama vya upinzani vya TLP,DP,UDP na Chausta.
“Masuala hayo ni kinyume cha maadili ya chama kifungu cha 10.1 (viii),(xii) na 10.2 (10),(xi) zenye kutoa maadili ya viongozi na sifa mahususi za viongozi kwa pamoja.
Hata hivyo,Kwapani aliliambia mwandishi kwa njia ya simu jana kuwa yeye hajapokea barua hiyo hadi sasa lakini akadai haukubaliani na agizo hilo kwakuwa mwenye uwezo wa kumsimamisha uenyekiti ni mkutano mkuu wa mkoa na si Katibu mkuu kama alivyofanya Mnyika.
“ Mimi sijapata hiyo barua hadi tunavyoongea lakini hata hivyo huyo Mnyika au Katibu mkuu wa Chadema Dk. Wilbrodi Slaa hawezi kunisimamisha Uenyekiti isipokuwa mkutano mkuu pekee….Lazima aelewe mimi siwajibiki kwake”,alisema Kapwani.
Kuhusu tetesi kwamba leo Kapwani alikuwa akimsubiri mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete ili ajiunge na Chama hicho katika uwanja wa Samora mjini hapa,Kapwani alisema si kweli kama jinsi ambavyo inadaiwa ila yeye bado ni mwana Chadema na ataendelea kukitumikia chama chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment