SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA (SHIVYAWATA), ambalo ni muungano wa vyama tisa vikuu vya kitaifa vya watu wenye ulemavu tofauti nchini vinampongeza Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Serikali ya Baraza La Mapinduzi Zanzibar 2010 – 2015.
Halikadhalika muungano huo wa vyama vinampongeza Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na chama chake Chama cha Wananchi (CUF) kwa kuchaguliwa kuwa mshindi wa pili kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), lakini pia kwa busara aliyoionyesha ya ukomavu wa kisiasa kwa kukubali matokeo na kuepusha vurugu ambazo zingeweza kutokea kama angeamua vinginevyo.
Kukubali kwake matokeo si kwamba kumeepusha vurugu tu, bali pia kumeepusha maafa na ongezeko kubwa la watu wenye ulemavu, lakini pia ifahamike kuwa machafuko yoyote yatokeapo waathirika na wahanga wakuu wanakuwa ni watu wenye ulemavu, akinamama, wazee na watoto, hivyo basi Mwenyekiti –SHIVYAWATA Lupi Maswanya Mwaisaka,kwa niaba ya watu wenye ulemavu nchini hatuna budi kumpongeza kwa busara aliyoitumia.
Alisema SHIVYAWATA kuwa ni matarajio yao kuwa Wazanzibar wataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoleta maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar kwa kuzingatia makundi yote ya kijamii wakiwemo watu wenye ulemavu, hususan katika kuzingatia mahitaji muhimu katika nyanja za huduma ya elimu, afya, ajira, miundombinu, ushirikishaji katika vikao vya maamuzi n.k.
Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wanawatakia kila la kheri Serikali mpya ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano na upendo na kuwaletea mabadiliko ya kiuchumi wananchi wa Zanzibar yatakayoleta maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment