Monday, 31 January 2011

MTIHANI KIDATO CHA SITA: WASICHANA MAPOSENI KUWAONYESHA KAZI WAVULANA

 Sehemu ya wahitimu 53 wa Shule ya Sekondari ya Maposeni wa Kidato cha Sita wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza sherehe ya Mahafali ya Pili 2011.

Mkuu wa Shule ya Maposeni Sekondari, Humari Mapunda akisoma taarifa ya maendeleo ya shule kwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya Pili ya kidato cha Sita 2011. 

BAADA ya wasichana kung’ara Kidato cha Nne 2010, nao wasichana wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Maposeni wamenena kuwaonyesha kazi wavulana katika mtihani ya Kidato cha Sita Mwaka 2011.


Hivi karibuni Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilitangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliyofanyika Oktoba mwaka jana yaliyoonyesha kuwa wasichana waliongoza kwa kiwango cha ufaulu.


Hata hivyo, matokeo hayo yameonyesha kuwa kiwango cha ufaulu katika mtihani huo kimeshuka kwa asilimia 22 ikiliganishwa na matokeo ya mwaka 2009 kuwa wasichana walifanya vizuri zaidi kuliko wavulana, alisema Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Joyce Ndalichako.


Wasichana hao wa Shule ya Sekondari ya Maposeni walisema hayo Ijumaa wiki jana katika Mahafali ya Pili ya Kidato cha Sita Mwaka 2011 yaliyofanyika Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma.


Baadhi ya wasichana waliongea na Nipashe ni Waridi Hyera na Selesia Kinundu walisema kuwa kama wasichana waliowatangulia walivyofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita mwaka jana nao pia watafuata nyayo kwa kufanya vizuri zaidi katika mtihani wao utakaofanyika tarehe 7. 2. 2011.


Historia inaonyesha kuwa shule hiyo wasichana 50 wa mara ya kwanza walifanya vizuri katika mtihani ya kidato cha sita 2010. Hivyo basi mwaka 2010 walifanya mahafali ya kwanza ya kidato cha sita na walikuwa ni wasichana tu.


Shule huyo ilianza kuwa na Advanced level April 2008, kwa hiyo wahitimu wa kwanza wa kidato cha sita walimaliza Februari 2010. Machaguo ya masomo wanayosoma hapa ni HGK na HKL. Wahitimu 50 wote walikuwa wasichana, matokeo yao yalikuwa mazuri sana kwani walipata daraja la I, II na III hivyo hakuna aliyepata daraja la IV na 0 mwaka jana.


Wahitimu wa mwaka huu ni 53 wa kidato cha sita kati ya wanafunzi 60 tulioanza kozi hiyo mwaka 2009, kwa sasa waluvana 35 na wasichana 18 nakufanya idadi ya wanafunzi kuwa 53.


Shule hii pia ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi nne ambao jumla yao ni 752. Kidato cha tano wapo 69 jumla 821 ya wanafunzi wote.


Katika risala ya wahitimu hao wa kidato cha sita mwaka 2011 kwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili, ilieleza kuwa wanafunzi walianza kidato cha tano wakiwa 60 ambapo wavulana walikuwa 38 na wasichana 22, upungufu huo umetokana na sababu zisizozuilika za kuhama,kutokana sababu za kiafya wanafunzi saba wasiweze kuhitimu ambao wavulana ni watatu na wansichana ni wanne.


Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la PADI, Iskaka Msigwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo aliwaasa wahitimu kushika huyu elimu kamwe wasichanganye mambo kwani ukimwi utawamaliza kabla hajamaliza elimu ya chuo endapo watafanikiwa kuchaguliwa kujiunga na elimu ya juu mwakani.


“Itakuwa ni kazi bure kwa wazazi au walezi wenu kuwaona mnakufa na ukimwi baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu pia serikali itakosa wataalamu baadae kwa sababu haiwezi kuwaajili watu walioathirika kwa ukimwi…. Kwa hiyo jihadhalini na ugonjwa wa ukimwi unaua” alisema.


Mkuu wa Shule hiyo Humari Mapunda katika taarifa yake aliyoisoma kwa mgeni rasmi alisema kuwa majukumu ya shule ni kutoa elimu ili kufanikisha malengo ya taifa, wanakumbana na vikwanzo mabalimabli, ikiwa ni pamoja na upungufu wa walimu katika masomo ya sanyansi kwa kidato cha 1-4 na mwalimu wa kiingereza kwa kidato cha 5-6, uchakavu wa majengo, ukosefu wa umeme kwa sasa wanatumia umeme wa jenereta ambalo huwashwa kwa msimu hususani vipindi vile vya mitihani.


Matatizo mengine ni ukosefu wa chanzo cha maji ya uhakika, ukosefu wa ukumbi wa chakula na upungufu wa matundu ya vyoo na upungufu ni 18, yaliyopo ni 24 wavulana 11 na wasichana 13, ukosefu wa majengo mawili ya maabara (physics na chemistry), upungufu wa nyumba za walimu zilizopo ni tano upungufu ni 25 (pia nyumba 3 hazijakamilika) na upungufu wa watumishi wasio walimu kama Boharia na Mhasibu.








No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...