Saturday, 5 February 2011

KAMATI YA KUSHUGHULIKIA MGOGORO WA IVORY COAST

Tanzania imeteuli kuwa moja ya nchi TANO katika kamati ya Umoja wa Afrika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Ivory Coast kati ya Rais anayemaliza muda wake Bwana Laurent Gbagbo na Bwana Alassane Outtara.






Nchi zingine kaatika kamati hiyo ni Chad, Mauritania, Nigeria na Afrika ya Kusini, nchi hizi zitaungana na nchi ya Burkina Faso ambayo tayari inashughulikia mgogoro huo.






Kamati hiyo imefanya mkutano wake wa kwanza tarehe 31, Januari 2011 mjini Addis Ababa ambapo imekubaliwa kuwa kila nchi itachagua mwakilishi wake katika kamati ndogo ya wataalamu ifikapo tarehe 3 Februari ambao watakwenda nchini Ivory Coast kuangalia na kutathmini hali ilivyo.






Baada ya hapo Kamati ya wataalamu watatakiwa kutoa taarifa na ushauri kwa viongozi ambao hatimaye watakwenda Ivory Coast na kukutana na viongozi hao wawili wanaogombea madaraka.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...