Na Mwandishi Wetu,
Ludewa
TUHUMA za ubadhilifu wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja zinazomkabili Askofu John Simalenga wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Southwest Tanganyika Njombe, umechukua sura mpya baada ya waumini wenye hasira kumzuia kuendesha Ibada Milo.
Dhahama hiyo ilimpata mchungaji huyo wa kiroho Oktoba 23, 2011katika Kanisa la Kung’aa kwa Bwana lililoko Mtaa wa Milo wilayani Ludewa mkoani Iringa, alikokwenda kuendesha Ibada ya Kipaimara.
Awali waumini hao walimsimamisha kazi mchungaji wa mtaa wa Milo Padre
Jophrey Mturo na kumnyima mshahara kwa madai kuwa ameshiriki ubadhirifu huo ndiyo maana amekuwa akimtetea Askofu huyo.
Hata hivyo, Padre Mturo alilazimika kufungasha mizigo yake siku hiyohiyo na kukimbilia Kijiji cha Mlangali kwa hofu ya kuvamiwa na waumini wenye hasira na kwamba anasubiri maelekezo ya Askofu kuhusu kupangiwa kituo kingine cha kazi.
Wakizungumza kanisani hapo waumini na viongozi wa mtaa huo walisema
wameamua kumzuia mlangoni Askofu Simalenga kutokana na dharau alizoonesha kwao kwa kukaidi kutoa maelezo kuhusu ni wapi amepeleka vifaa vya hospitali yao vilivyotoka Ujerumani mwanzoni mwa mwaka huu.
Katika madai yao waumini wanadai Askofu Simalenga pamoja na wenzake, mwanzoni mwa mwaka huu walipokea kontena lililo sheheni vifaa vya hospitali yao na vifaa vingine vya utabibu zikiwemo kompyuta 154 vyote vikiwa na thamani ya shilingi bilioni moja (1bn/-).
Michael Mwinuka ni Katibu wa Mtaa na mwalimu katika Kanisa la Kung’aa kwa Bwana Milo. Kwa upande wake alisema waumini wamechoshwa na ubabe
wa Askofu Simalenga ndiyo maana wameungana na kumtaka afanye kikao
kwanza ndipo aendeshe Ibada.
Mwinuka amesema yapo mambo mawili yaliyo pelakea waumini kumzua Askofu kuingia kanisani ikiwemo kuja kutoa Kipaimara kwa watoto ambao
hawamaliza mafundisho kwa mujibu wa taratibu za kanisa.
“Watoto wanatakiwa kuhudhuria mafundisho kwa kipindi cha mwaka mzima, lakini wamemaliza miezi miwili tu jambo lililopelekea wazazi kuwazuia watoto wao wakidai kuwa wangepata kipaimara bila kukomaa kiimani,”
alisikitika Mwinuka.
Alisema idadi ya watoto waliokuwa wanahudhuria mafundisho ya kipaimara walikuwa 43 kwa muda wa miezi miwili, lakini baada ya wazazi kuwazuia watoto wao walibaki watoto 8 watatu wakiwa watoto wa padre.
Akaongeza kuwa waumini wamechoshwa na uovu, ubabe, udharimu na tabia chafu za Askofu Simalenga kwani amefanya kanisa kama mali yake binafsi jambo ambalo linawatia kichefuchefu waumini na kwamba kama angeacha kiburi tusingefikia hatua hii.
Askofu Simalenga alipata wakati mgumu na kulazimika kujificha ndani siku nzima hata Polisi wa Kituo cha Mlangali walipokwenda kutaka kujua kulikoni hakuwa tayari kujitokeza mbele ya viongozi na waumini wa kanisa hilo, akidai atapanga siku nyingine.
Mchungaji Christopher Mtikila akizungumza kijijini hapo alikokwenda msibani alisema amefurahishwa na ujasiri wa waumini wa Milo kwani inaonesha wameanza kuzitambua haki zao na kuchoshwa na ufisadi wa kiongozi wao na kuwataka Watanzania kuiga hatua hiyo.
Mimi niko tayari kutoa ushirikiano kwa kuonesha mahali zilikouzwa, kompyuta, X-Ray na vifaa vingine kwa sababu aliyenunua yupo anafahamika na anakubali kwanini kuwazungusha waumini kiasi hicho? aliuliza Mtikila
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Milo Ananias Mwinuka alikiri kutokea kwa mgogoro huo wa muda mrefu na kwamba siku ya tukio aliitwa na kuhudhuria kikao kati ya polisi, waumini na viongozi, lakini Askofu alikataa kuhudhuria jambo lililo shangaza wengi. Alimtaka Mchungaji huyo kumaliza mgogoro kwa njia ya mazungumzo siyo ubabe.
Naye Msaidizi wa Askofu Vicar General Kenani Michael Mlelwa akizungumza kwa njia ya simu alithibitisha bosi wake kuzuiliwa kuendesha Ibada Jumapili ya Oktoba 23 mwaka huu, lakini akawataka waumini kuwa na subira.
Alikiri kuwepo kwa malalamiko dhidi ya Askofu Simalenga kwa muda mrefu na kusema kuwa madai hayo siyo ya kweli na kuongeza kuwa Askofu atapanga kuonana na waumini hao siku nyingine watakapokuwa wamepunguza jazba.
Mgogoro wa kumtuhumu Askofu Simalenga juu ya ubadhilifu wa vifaa vya
kanisa ulianza kufukuta mwanzoni mwa mwaka huu na kila alipotakiwa kutoa ufafanuzi alikaidi maombi ya waumini wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment