Na Friday Simbaya
KAMPUNI inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya Urani ya Mantra Tanzania Ltd iliyopo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imesema itatoa ajira kwa vijana zaidi 1600 kutoka vijiji mbalimbali baada ya kupatiwa kibali cha kuanza kazi ya uchimbaji.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mjeolojia Mkuu kampuni hiyo Bw. Emmanuel Nyamusika wakati alipokuwa akitoa taarifa mbalimbali kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma (RPC) walipotembelea eneo la mgodi wa madini hayo kwa lengo la kujiridhisha baada ya kupata malalamiko kutoka vijijini vilivyo jirani mgodi huo.
Alisema,licha ya kutoa ajira hizo kwa vijana,kampuni hiyo imeshaanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali ya awamu ya nne kwa kuwahamasisha wakazi wa vijiji jirani na mgodi huo kuanzisha vikundi vya kiuchumi na tayari imeshaanza kutoa fedha za kuwawezesha wanavikundi hao kuifanya shughuli za maendeleo kama ufugaji wa kuku wa mayai na nyama.
Alisema,lengo la kufanya hivyo ni kutaka wananchi hao kunufaika na uwepo wa mgodi huo na pia kuunga mkono juhudi za serikali.
Alisema, mpaka sasa bado wanaendelea na kazi ya utafiti kwa eneo lote lilokusudiwa ambalo ni km za mraba 332, lakini wameshindwa kufanya utafiti wao kwa eneo lote ilo kwa sasa na kufanikiwa kufanya utafiti wao kwa km za mraba 100.
"Tunategemea kuendelea na utafiti katika maeneo yaliyobaki baada ya kupata kibali cha kazi ya uchimbaji,lengo letu ni kutaka kuyafikia maeneo yote ya mradi huu,hata kuongeza ukubwa wa eneo kwani tunaamini pori ili lina hazina kubwa ya madini ya Urani,"alisema,
Pia ameiomba serikali,kusaidia upatikaji wa kibali cha uchimbaji ili waanze kutekeleza baadhi ya mipango yake ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika vijiji jirani na eneo la mgodi kwa kuwa hairuhusiwi mtumshi kuishi kambini na familia yake.
Akizungumzia kuhusu uharibifu wa mazingira, Bw.Nyamusika aliwatoa shaka waandishi wa habari kusema kuwa watakuwa na utaratibu wa kufukia mashimo hayo ,na kupanda nyasi na baadhi ya mimea itakayosaidia kurudisha maeneo hayo katika hali yake ya kawaida.
Ziara ya waandishi wa Mkoa wa Ruvuma (Ruvuma Press Club) kwenye mradi wa Mkuju River Project ulifanyika tarehe 8/12/2012. Mradi huo hupo umbali wa zaidi kilemeta 50 kutoka Kijiji cha Likuyu Sekamaganga.
Hata hivyo, ziara ya waandishi wa habari kwa kampuni ilikuwa na lengo la kuhufahamu mradi wa Mkuju River Project; kujifunza kuhusu madini ya urani na vifaa vya mionzi na mahusiano kati ya jamii zilizopo na kampuni.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Ruvuma Press Clubu ,Andrew Kuchonjoma alimshukuru Mantra Tanzania Limited pamoja uongozi wa Wilaya ya Namtumbo kwa niaba ya waandishi wa habari kwa kuandaa ziara, na alisema ziara ilikuwa na mafanikio.
"Tumepata elimu juu ya ukweli kuhusu vifaa vya madini ya urani na mionzi na dhana potofu kuhusiana mradi Mkuju River Project. Wote tunahitaji ni kwenda nyumbani na kujaribu kuelimisha jamii katika maeneo yetu kuhusu ukweli wa urani, "alisema Kuchonjoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment