Dkt. Slaa alisema kuwa watu wengi waliofikisha miaka kumi na nane (18) na waliopoteza shahada hizo ama kwa kuuza au kupoteza hawatashirika kupigakura ya maoni ya katiba.
Hayo yalisema leo wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Tamasha vilivyopo Namihoro, wilayani Songea vijijini mkoani Ruvuma, wakitokea Mbamba Bay na Mbinga, ikiwa ni kuashilia mwanzo wa opresheni M4C PAMOJA Daima inayofanyika nchini nzima.
Alisema ili watu wengi waweze kushiriki kupigakura ya maoni ya katiba kikamilifu ni lazima daftari ya wapigakura nchini liboreshwe.
“Tunaiomba serikali kupitia Tume ya Uchaguzi Nchini (NEC) ianze zoezo la kuboresha daftari ya wapigakura ili watu wengi washiriki katika kupigakura ya maoni ya katiba na hatimaye Uchaguzi Mkuu wa 2015,” alisema Dkt. Slaa.
Aliwaomba wananchi wa Jimbo la Peramiho kushiriki kikamilifu katika chaguzi za serikali za mitaa zinazo tarajia kufanyika mwaka huu ili kuweza kuchaguwa upinzani kikiwemo chama cha Chadema.
Alisema kuwa kwa sasa maisha ya wanachi ni magumu pamoja kwamba nchi imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi lakini wananchi wake bado ni masikini kwa sababu ya viongozi kukosa moyo wa uzalendo.
Gharama za maisha inapanda kila siku hasa gharama za matibabu hospitali hususan hospitali binafasi ni kubwa na ukizingatia Peramiho haina hospitali ya serikali ambaye ni mkombozi wa wanyenge.
Alisema kuwa endapo chama chake cha Chadema kitafanyikwa kushika madaraka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kitu cha kwanza ni kuuza ndege ya serikali amabye anatumia na rais na kununua helikopta nyingi zinazo fikika kila mahala kuliko ndege ya rais inayotua viwanja sita tu.
Aiongeza kuwa kutumia ndege ya serikali ni gharama kuliko kutumia helikopta kwa sababa ni rahisi kufanya mikutano kumi na nne kwa siku kwa sababu ya kutumia helikopta.
MALENGO YA OPERESHEN
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema operesheni hiyo imezingatia mwaka 2014 kuwa na historia ya matukio ya kisiasa nchini, ambayo chama kinahitaji kujipanga kukabiliana nayo.
Aliyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na Bunge Maalumu la Katiba linalotarajiwa kuanza rasmi mwanzoni mwa mwezi ujao.
Hivyo, alisema chama kimeona kuwa kuna ulazima wa kuliandaa Taifa kwa ajili ya kulikabili tukio hilo.
Alisema matukio mengine ni uchaguzi wa serikali za mitaa na kura ya maoni, ambayo itapigwa na wananchi kuamua ama kuikubali au kuikataa rasimu ya pili ya katiba mpya.
Kutokana na hilo, Mbowe alisema wanatumaini kuwa daftari la kudumu la wapigakura litatumika katika kuendesha kura ya maoni.
Hivyo, alisema wameona ni lazima waliamshe Taifa kuhusu kujiandikisha katika daftari hilo.
Alisema tangu mwaka 2010, daftari la kudumu la wapigakura halijaboreshwa.
Kutokana na hali hiyo, alisema itakuwa ni ndoto za serikali kufikiria kwamba Watanzania watarudi kuitumia katiba ya mwaka 1977 inayotumika hivi sasa baada ya kuwa tayari wamekwishaikataa.
Mbowe alisema matukio mengine ya kisiasa yanayotarajiwa kujiri mwaka huu, ni uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 27 nchini.
Mbowe alisema katika mwaka huu pia kunatarajia kufanyika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Kalenga kuziba nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha Dk. Mgimwa.
Alisema pia katika mwaka huu watakuwa na uchaguzi wa ndani ya chama, hivyo wameona ulazima wa kuwaandaa wana-Chadema kushiriki uchaguzi huo.
Alisema pia Watanzania watakuwa na uchaguzi mkuu mwakani, hivyo wameamua kuutumia mwaka huu kukazia maandalizi kwa ajili ya ushiriki wao katika uchaguzi huo.
Mbowe alisema watatumia fursa hiyo kuibua kashfa na mambo yote yanayowakera wananchi katika maeneo yao.
Kwa mujibu wa Mbowe, operesheni hiyo ambayo itakuwa ya wiki mbili, itaendeshwa kwa njia ya mikutano ya hadhara na ya ndani.
No comments:
Post a Comment