Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) akiteta jambo na mmoja wa waombolezaji wa msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Moshi Chang'a wakati wa maziko katika makaburi ya Mtwivilla yaliopo Kihesa Manispaa ya Iringa mkoani Iringa leo.
Mwandishi wa habari wa www.fridaysimbaya.blog.com, Friday Simbaya (kushoto) akipata taarifa kutoka kwa mtoto wa mwisho wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, marehemu Moshi Chang'a, Hamis Moshi Chang'a wakati wa maziko katika makaburi ya Mtwivilla yaliopo Kihesa Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa leo.(Picha na Sagine Edward Majura)
Mtoto mwingine wa marehemu Moshi Chang'a, Shabaan Mosji akifarijiwa na baadhi ya waombolezaji nyumbani kwa baba yake Kihesa kwa Mwachang'a baada ya maziko leo.
Mtoto wa mwisho wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Moshi Chang'a, Hamis Moshi Chang'a (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya waombolezaji makaburini leo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Christine Ishengoma (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo wakifurahia jambo nyumbani kwa marehmu Moshi Chang'a leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa (RPC), Kamnshina Msaidizi wa Polisi (ACP), Ramadhani Mungi (katikati) akifuatilia maziko kwa makini katika makaburi ya Mtwivilla Kihesa leo. RPC Mungi alikuwa ni mmoja ya viongozi wa polisi walioudhulia mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, marehemu Moshi Chang'a.
Sheikh wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Athuman Amani kutoka Msikiti wa Masijid N-aor akitoa mawaidha na shukurani kwa niaba ya waumini wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa baada ya mazishi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, marehemu Moshi Chang'a makaburini leo mchana.
Sheikh wa Wilaya ya Iringa mjini, Issa Ngwele akiongoza dua wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Moshi Chang'a,ambaye ameacha watoto watano, watoto wakiume wa tatu na wawili wa kike.
Umati wa waombolezaji makaburini.
Afisa Utalii wa TANAPA katika Nyanda za juu Kusini, Risala Kibongo na Askofu wa KKKT Iringa, Mdegella wakifurahia jambo nyumbani kwa marehemu Moshi Chang'a.
Askofu Mdegella na Mwenyekiti wa Wilaya ya Iringa Mjini (CCM), Abeid Yusufu Kiponza. Askofu Mdegella ashikilia msimamo ule ule wa serikali mbili, asema kamwe hatabadilisha msimamo wake.
Kaimu Katibu wa Mkoa CCM Iringa, Miraji Mtaturu (kushoto) akitoa salamu kwa niaba ya chama mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro wakibadilishana mawazo na baadhi ya waombolezaji nyumbani kwa marehemu Moshi Chang'a.
Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani mwamwindi (katikati) akitoa salamu.
Baadhi ya waombolezaji wakifuatilia maziko.
(PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA)
Na Friday Simbaya
Mamia ya wakazi wa mji wa Iringa wamzika aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, marehemu Moshi Chang’a katika makaburi ya Mtwivilla Manispaa ya Iringa mkoani Iringa leo mchana.
Mkuu wa Wilaya Chang’a alifariki dunia Aprili 20, 2014 kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Shughuli ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu Chang’a kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ilifanyika jana mchana nyumbani kwake Mbagala, Kibonde Maji, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Marehemu Chang’a amezikwa leo Kihesa, Manispaa ya Iringa ambapo Serikali imewasilishwa na Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia.
Marehemu ameacha watoto watano, wa kike watatu na wa kiume wawili, Mungu alaze roho ya marehemu mahala pema. Amina.
No comments:
Post a Comment