Kuzaliwa kwa utawala wa kinasaba sio jambo jepesi kubashiri.
Lakini
wananchi wengi wa Zimbabwe kwa sasa wanaonekana kushawishika kuwa kuna
uwezekano wa familia ya Mugabe kuingia katika orodha hiyo ya
kurithishana madaraka.
Rais Mugabe ana umri wa miaka 90. Mke wake, Grace, ana umri wa miaka 49.
Uvumi wa
kurithishana madaraka umekuwa gumzo la kisiasa nchini Zimbabwe kwa miaka
mingi, lakini Grace Mugabe katika miaka ya karibuni ameibuka kama mtu
ambaye ataweza kumrithi mumuwe madaraka ya uongozi wa nchi ya Zimbabwe.
Watu wa nje
wamesikia tabia ya mke wa Rais Mugabe ambaye ni karani muhtasi wake wa
zamani kutuhumiwa kufanya manunuzi yasiyo na mpangilio na katika tukio
lingine kumpiga ngumi mwandishi wa habari wa Uingereza huko Hong Kong;
na kufanya mambo mengine ambayo yanavuka mpaka kama mke wa kiongozi.
Vyombo vya
habari vya Zimbabwe, kwa kulinganisha vimedhamiria kumjenga Bi Grace
Mugabe kuwa mtu wa kujitolea kwake katika kazi za kijamii.
Wazo la
"Rais Grace" kwanza alipata fursa hii mwezi Agosti wakati Bi Mugabe –
mwanafunzi katika siasa, bila kutarajiwa aliidhinishwa kama kiongozi
mpya wa Umoja wa Wanawake wa chama tawala cha Zanu-PF - jukumu ambalo ni
kubwa na litathibitishwa na mkutano mkuu wa chama hicho mwezi Desemba
2014.
Moto
ulichochewa mwezi huu wakati mke huyo wa Rais Mugabe alipotunukiwa
heshima ya kuwa Dokta Mugabe – Alitunukiwa shahada ya PhD katika
sosiolojia miezi miwili baada ya kujiandikisha katika chuo kikuu cha
Zimbabwe, na tasnifu yake haipo katika hifadhi ya mtandao wa chuo kikuu
hicho.
Uchambuzi wa kina unaonyesha kuwa Bi Mugabe hana nafasi ya kuwa rais, na anatumiwa na kundi moja ndani ya chama cha Zanu-PF.
"Ni rahisi
kuelezea. Ameletwa kama njia ya kumzuia Joyce Mujuru kwa njia yoyote
ile," anasema mchambuzi mwandamizi wa masuala ya kisiasa Ibbo Mandaza.
Bi Mujuru ni makamu wa rais na anaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kumrithi Rais Mugabe.
"Wakati mume
wake akiondoka ndiyo mwisho wake wa kazi ya uanasiasa, kama kweli kuna
kazi ya aina hiyo" anasema mchambuzi wa masuala ya siasa nchini
Zimbabwe,anasema Ibbo Mandaza, akitupilia mbali wazo la kuendelea kuwa
na utawala wa familia ya Mugabe.
Nadharia
nyingine ni kwamba Rais Mugabe anamjenga mke wake ili kuyayumbisha
makundi yote ndani ya chama cha Zanu-PF, na kuimarisha nafasi yake ya
urais.
Dewa Mavhinga, kutoka Human Rights Watch, anaamini kuwa rais amefanya kosa kubwa kumleta mtu ambaye hana ujuzi wowote wa siasa.
"Inaonyesha kuwa Rais Mugabe hamwaamini mtu yeyote karibu naye"Dewa Mavhinga.
CHANZO: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment