Mchungaji Peter Msigwa |
Akiwa na Makamu Mwenyekiti Bavicha, Patrick Ole Sosopi |
Sehemu ya watu waliojitokeza katika mkutano huo |
Wakionesha ishara ya chama chao |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kimelitaka jeshi la Polisi kudhibiti misafara mirefu ya magari na
pikipiki, na aina yoyote ya maandamano yatakayopangwa na Chama cha Mapinduzi
(CCM) Mkoa wa Iringa wakati wa mapokezi ya katibu wake mkuu, Abdulahman Kinana.
Oktoba 6-11, mwaka huu Kinana atakayeambatana
na Katibu Itikadi na Uenezi wa chama hicho Nnape Nauye anatarajia kufanya ziara
ya kukijenga chama hicho na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika wilaya
zote za mkoa wa Iringa.
Ombi hilo limekuja baada ya jana Jeshi la
Polisi kuwadhibiti wafuasi wa chama hicho wa mjini Iringa kumlaki kwa
maandamano ya magari na pikipiki, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA)
jimbo la Isimani, Patrick Ole Sosopi ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa Bavicha.
Sosopi aliyekuwa na Mchungaji Peter
Msigwa wakitokea jijini Dar es Salaam kulikofanyika chaguzi mbalimbali za
kitaifa za chama hicho, walipokelewa katika eneo la Igumbilo na viongozi wachache
wa chama hicho baada ya Polisi kudaiwa kuwazuia wafuasi wao kuwapokea kwa
misafara ya magari, bodaboda na maandamano.
“Tumetii maelekezo ya Polisi, vijana wetu
wa bodaboda wamezuiwa kutupokea; ili haki itendekea tunataka Kinana na timu yake
watakapoingia mjini Iringa, misafara yao isiwe na maandamano ya watu, pikipiki
wala magari,” alisema Mchungaji Msigwa katika mkutano wao mkubwa uliofanyika
katika kata ya Kihesa mjini Iringa.
Mchungaji Msigwa alisema watashangaa na
kuchukua hatua endapo Polisi itairuhusu CCM kuwa na maandamano na misafara ya
magari na pikipiki.
Naye Mwenyekiti wa Chadema wa Jimbo la
Iringa Mjini, Frank Nyalusi alisema; “Kinana atakuwa mjini Iringa Oktoba 11,
tukiona bodaboda wa CCM wako katika msafara wake nasi tutaingia barabarani
tukiwa na wafuasi wetu madereva wa bodaboda na kufanya maandamano yasio na
kibali.”
Makamu Mwenyekiti wa Bavicha Ole Sosopi
alisema; “mimi ni kiongozi wa kitaifa, niliongea na Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Iringa kuhusu ujio wangu Iringa na mipango ya wafuasi wa Chadema kunipokea
kwa shamrashamra. Nashangaa amekataa.”
Alisema kuyazuia maandamano ya Chadema na
kuruhusu ya CCM kutadhihirisha jinsi Polisi wanavyokibeba chama hicho tawala.
Alisema wakati wakijiandaa kuchukua Dola wanataka
kuona wanashindana katika uwanja sawa wa kisiasa kwahiyo hawatakubali kuona
jashi la Polisi linaruhusu maandamano katika misafara ya Kinana wakati kwao
linakataa. (Crediti to Bongeleaks)
Itaendelea……………………………..1
No comments:
Post a Comment