Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete ametunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa Kitanzania 23 miongoni mwa
maafisa 437 wa kundi la 53/13 – Kongo. Kundi hilo liliwajumuisha maafisa wa
kitanzania wapatao 23 na wahitimu 414 kutoka Kongo.
Jumla
ya wanajeshi 414 kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo leo (18/10/2014 wamehitimu mafunzo ya Uafisa katika chuo
cha maafisa (TMA) Monduli baada ya
kufanya kozi kwa muda wa mwaka mmoja.
Maafisa
hao wanafunzi kutoka Kongo walipata mafunzo hayo pamoja na maafisa watanzania
23 waliohitimu leo na kupata kamisheni ya cheo cha luteni usu baada ya kula
kuapa mbele ya Mhe. Rais Dkt Jakaya Kikwete.
Tofauti
na kamisheni zingine kwani pamoja na Mhe. Rais Kikwete aliweza kutoa Kamisheni
kwa maafisa wapya wapatao 23 .
Aidha,
leo hii kitu ambacho ni kigeni vijana kutoka kongo walihitimu pasi kutunukiwa
kamisheni kwani kulingana na taratibu maafisa wa kongo wanapaswa kupewa kamisheni na Rais na
wakiwa katika ardhi yao, hivyo wahitimu hao watakapewa kamisheni nchini mwao.
Akitoa
shukurani kwa Rais Kikwete wa Tanzania, Rais Joseph Kabila ambaye alishuhudia
maafisa wake wakihitimu mafunzo hayo, alisema anawashukuru kwa kukubali kutoa
mafunzo kwa maafisa hao.
Pia
alisema anaamini atakuwa amepata makamanda wazuri watakaosaidia kuimarisha
usalama nchini mwao na pia kuondoa maadui wanaohatarisha amani nchini Kongo.
Miongoni
mwa viongozi waliohudhuria sherehe hizo Wazri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Dkt
Hussein Ali Mwimnyi, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.
Bernard Membe, Katibu mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Waziri Mkuu Mstaafu na mbunge
wa Monduli, Mhe. Edward Lowasa, Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Bw. Magesa Mlongo,
majenerali, majenerali wastaafu, na mabalozi wa kijeshi wanaoziwakilisha nchi
zao hapa nchini.
kwa
upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Naibu Waziri Mkuu na waziri wa
Ulinzi, Alexander Luba Ntambo, na Waziri wa Mambo ya Nje, Raymond Tshibanda
N’tungamulongo, Balozi wa Kongo nchini Jean Pierre Juma Alfani, Mkurugenzi wa
Idara ya Usalama Kahimbi Delphin na Mkuu wa Mafunzo, ya Kijeshi, brigedia Jenerali Aguru Mamba Maurice.
No comments:
Post a Comment