Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo (kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuhuisha rejesta ya wakazi katika mitaa leo ofisini kwake. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Na Friday Simbaya,
Iringa
Manispaa ya Iringa
kupitia waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa imeridhia kufutwa kwa vijiji
na kubakiwa na mitaa, hivyo Manispaa itakuwa na mitaa 192 kwa ongezeko la mitaa
43 (mitaa ya zamani 149).
Akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa,
Theresia Mahongo alisema kuwa mitaa 14 iliyotokana na maombi ya kugawana mitaa
iliyoonekana kuwa na eneo kubwa na mitaa 29 iliyotokana na vitongoji kuitwa
mitaa kutokana na vijiji kufutwa.
Aidha, alivitaja
vijiji saba (7) vilivyofutwa kuwa ni Igumbulo, Nduli, Kigonzile, Mgongo na
Itamba. Katika tangazo la
serikali namba 300 la tarehe 22.08.2012 limeelezea maeneo ya utawala katika
mamlaka za serikali za mitaa mwaka 2014.
Kwa kuzingatia tangazo
hilo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imekubaliwa kuwa na kata 18, kata mpya
zikiwa ni kata ya Igumbulo inayotokana na kugawanywa Kata ya Ruaha na Kata ya
Mkimbizi ambayo imetokana na kugawanywa Kata ya Mtwivila.
Kuhusu kuhuisha rejesta
ya wakazi katika mitaa mkurugenzi huyo aliwataka wananchi wote wa Manispaa ya Iringa
wajitokeze kujiandikisha katika rejesta ya wakazi katika mitaa husika.
Alisema kuwa daftari la
wakazi la mtaa ni kumbukumbu ambayo inataarifa zote muhimu za wakazi wa mtaa na
vitongoji wa eneo husika. Taarifa hizo ni kama jina la mkazi, umri, mtaa
anaoishi, idadi ya watoto kama wapo n.k.
“Rejesta ta wakazi
ilianzishwa chini ya sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 ambapo inataka
wakazi wote wawe wameandikishwa ikiwa umehamia, umehama au mtoto amezaliwa
laizama taarifa ziwepo kwenye daftari la wakazi la mtaa,” alifafanua Mahongo.
Alisema umuhumu wa
kuhuisha taarifa katika rejesta za wakazi pamoja na mambo mengine itasaidia
kufahamu idadi ya wakazi katika kila mtaa, na itasaidia pia katika kuandaa
mipango ya manispaa kwa kufahamu idadi ya wakazi ulionao na mahitaji yao katika
mipango ya maendeleo.
“wanatakiwa kusimamia
zoezi hili kwenye kata zetu ni watendaji wa mitaa na wa wenyeviti wa mitaa,
kwani hawa ndio wanafahamu watu wake kwenye mtaa husika na ndio wanatambulika
katika mfumo wa serikali kwenye ngazi ya mtaa,” alielezea.
No comments:
Post a Comment