Baadhi ya makazi duni eneo la Katanga nchini Uganda. (PICHA KWA MSAADA WA MTANDAO)
Na Friday Simbaya, Iringa
Ikiwa ni katika
kuaadhimisha siku ya makazi duniani Shirika la nyumba la taifa (NHC)
katika juhudi ya kuunga mkono serikali ili kuondokana na makazi duni nchini
lina mpango wa kujenga jumla ya nyumba 15,000 mpaka kufikia mwaka 2014/15.
Akiongea na THE SCOOP kwa njia ya simu Meneja wa
Huduma kwa Jamii (CSR), Muungano Saguya alisema shirika la nyumba lina mpango
wa kujenga jumla ya nyumba 15,000 ambapo nyumba 5,000 kati hizo zitakuwa za gharamu nafuu, wakati
nyumba 10,000 zitakuwa za bei ya kati na juu.
Alisema mpaka sasa shirika limeshajenga jumla ya
nyumba 1,227 za gharama nafuu na kuongeza kuwa Tanzania ina uhaba wa makazi 3,000,000 kwa ongezeko laki mbili kwa kila mwaka.
Alisema kuwa kuboresha makazi mijini shirika
limejikita zaidi kwenye uboreshaji makazi mijini (urban renewal) kwa
kubadilisha taswira za miji nakuifanya iwe namuonekano mpya.
“Hii ni pamoja na kubomoa majengo ya zamani na kujenga
majengo mapya yenye viwango vyote vya usalama (safety),” aliongea meneja wa
huduma kwa wateja huyo.
Kauli mbiu ya siku ya makazi duniani mwaka huu ni;
Sauti kutoka makazi duni.
Shirika katika kutatua tatizo la uhaba wa makazi
nchini unakadiriwa kufikia nyumba 3,000,000 kwa kujenga nyumba bora, nafuuna za
kisasa zitakazosaidia kupunguza upungufu wa makazi na kuleta mandhari bora mijini.
Hata hivyo, meneja wa huduma kwa jamii wa shirika la
nyumba taifa alitoa rai kwa halmashauri za miji kutoa ardhi kwa gharama nafuu
ili iweze kujenga nyumba bora na nyingi zaidi.
Siku ya makazi duniani uadhimishwa kila jumatatu ya
kwanza ya mwezi oktoba kila mwaka.
Na nchi wanachama wa umoja wa mataifa chini ya
uratibu wa shirika la makazi duniani (UN-HABITAT) huadhimishasiku hii kwa njia
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafakari hali ya makazi katika nchi husika na
kupanga mikakati ya kukabiliana na changamoto za makazi.
No comments:
Post a Comment