Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth
Mwanyika (kushoto) akitia saini mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya
Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM) Awamu
ya IV kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi
wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth
Mwanyika (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa
Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV waliosaini leo jijini
Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth
Mwanyika (kushoto) akishukuru Serikali ya Finland kwa ushirikiano mzuri
wanaoendelea kuipa Tanzania mpaka sasa na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika
katika malengo yaliyokusudiwa. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka
Antila.
Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila (kulia)PFM akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) na kuipongeza
kwa kusimamia fedha za umma na kuwa na uongozi unaosimamia utawala wa
kidemokrasia, uchumi imara, ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo na
hivyo kupunguza umasikini. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dae es salaam
wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa
Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV. Kushoto
ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika.
Na Eleuteri Mangi
-MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imepokea Sh. Bilioni 10.1 ambazo ni sawa na EURO milioni
4.8 kutika Serilkali ya Finland ikiwa kwa lengo la ushirikiano wa Mpango wa
Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV.
Mkataba wa makubaliano
hayo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi.
Doroth Mwanyika kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Finland nchini Bi.
Sanikka Antila.
Bi. Doroth amesema kuwa
Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya nne ametanguliwa na
Awamu ya I hadi III ambapo awamu hizo zimeonesha mafanikio mbalimbali nchini.
Mafanikio hayo ni
pamoja na ongezeko la ukusanyaji wa mapato kutoka Sh. Bilioni 390 mwaka
2009/2010 hadi zaidi ya Sh. Bilioni 700 kwa mwezi mwaka 2013/2014 na kuboresha
mifumo ya kifedha kwa kutumia mifumo ya kielektroniki kwa kulipa moja kwa moja
kwenye akaunti husika.
Bi Doroth metaja
mafanikio mengine kuwa ni ubureshwaji wa utendaji watumishi wanaosimamia
masuala ya mpango wa PFM kupitia Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za
Serikali (CAG) na utendaji kazi mzuri wa kamati za Bunge zinazohusika na
ufuatiliaji wa matumizi ya Fedha za umma.
Aidha, Bi. Doroth
ameishukuru Serikali ya Finland kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kuipa
Tanzania na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa
katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kupunguza umasikini nchini.
Naye Balozi wa Finland
nchini Bi. Sanikka Antila amesema kuwa usimamizi mzuri wa fedha za umma (PFM)
umeifanya nchi yake kuongeza fedha kwa ajili ya mpango huo.
“PFM ni muhimu kwa
utawala wa kidemokrasia, uchumi imara, ufanisi katika matumizi ya rasilimali
zilizopo na hivyo kupunguza umasikini” alisema Bi. Sanikka.
Ufanisi wa usimamizi
mzuri wa fedha za umma umewezesha ufanisi wa malighafi zilizopo nchini katika
kuboresha elimu, kutoa huduma bora za kiafya, kuongeza mazao ya kilimo na
kuendeleza utalii.
Mpango wa PFM upo
katika awamu ya nne na ulianza 2012 na unatarajiwa kuishia 2017 ambapo awamu ya
I hadi III ilianza 1998 na kumalizika 2012, Finland imekuwa nchi ya sita
mhisani katika kusaidia mpango huu wa mageuzi.
Nchi nyingine wahisani
ni pamoja na Canada, Ujerumani Ireland na Uingereza.
No comments:
Post a Comment