Tuesday, 28 October 2014

UGULUMO: TUTUMIE MITANDAO YA KIJAMII KWA MAENDELEO NA KIUCHUMI

 Mwanzishi wa Kundi la Matukio Daima Francis Godwin ambaye ni admin wa kundi hilo akitoa historia ya kundi hilo. 

MA MC WETU SIKU HIYO

 Ukumbini VETA


Mwanakundi Pamela Mollel kutoka Arusha akisoma risala kwa mgeni rasmi.


Mratibu wa Spanest ambao ni Mradi wa Kuboresha Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST), Godwell Ole Meing’ataki akitoa salama.



Enock Ugulumo wa Chuo cha Iringa Kitivo cha Biashara ambaye pia alikuwa ndio mgeni rasmi akitoa hotuba. (Picha zote Friday Simbaya)



Na Mwandishi Wetu, Iringa

Mitandao ya kijamii ni mizuri katika kuhabarisha umma endapo inatumiwa kulingana na madhumuni iliyotengenezwa, kwani ina nguvu ya kusambaza habari kwa haraka na kwa wakati hapa duniani.

Haya yalisemwa na Enock Ugulumo wa Chuo cha Iringa Kitivo cha Biashara ambaye pia alikuwa ndio mgeni rasmi hivi karibuni wakati sherehe ya WANACHAMA WA MATUKIODAIMA iliyofanyika Ukumbi wa VETA.

Kundi hili lilianzishwa na Francis Godwin ambaye ni admin wa kundi hili ambalo limegawanyika katika makundi mbali mbali likiwemo kundi la Matukiodaima mchanganyiko, kundi ambalo linashughulika na matukio na mijadala mbali mbali , kundi la Siasa Kali ambalo linajumuisha viongozi mbali mbali mbali wa kiasiasa wakiwemo mawaziri ,wabunge ,viongozi wa vyama vya siasa na wapenzi na wasio kuwa wapenzi wa vyama mbali mbali za siasa lengo ni kuangazia masuala mbali mbali ya kisiasa za ndani ya nchi na nje ya nchi .

 Alisema pamoja na umuhimu wa mitandao hii ya kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao hujiona kuwa wameendelea katika ulimwengu wa kisayansi na teknolojia kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo kinyume na malengo kwa kutumia kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama wa maeneo muhimu ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.
 “Watu hawa kwa jina la kisayansi na teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au Wezi wa mitandao kwa kisawahili, na wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao ya kuingilia mitandao mingi iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa wakitumika katika shughuli za kigaidi ulimwenguni, alisema”.
 Alisema kuwa ili kujiweka salama dhidi ya wezi wa mitandao, basi tujitahidi kutoa taarifa zozote za kiusalama kwa vyombo vya usalama yaani Polisi au kupeleka malalamiko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pindi tunapoona taarifa za uvunjwaji wa sheria za matumizi ya mitandao, mfano mtu akiona kuna hitilafu katika taarifa za muamala wa fedha zake katika akaunti yake ya benki fulani basi atoe taarifa kwa benki husika ili wao waweze kutafuta tatizo na kutoa ufumbuzi.
Pamoja na haya yote Watanzania wamehimizwa kuacha matumizi mabaya ya mitandao ya jamii ikiwemo kuweka picha za utupu, kusababisha ugomvi, kuwahimiza wengine kwa mambo yasiyo ya kweli, kupotosha jamii na kuvuruga maendeleo.
Alisema matukio yanayofanyika katika mitandao hiyo na kuleta athari ni utapeli, kulipiza kisasi na ugomvi unaoanzia mitandaoni na kuendelea hadi kwenye uhalisia.

RISALA YA WANACHAMA WA MATUKIODAIMA KWA MGENI RASMI -26/10/2014


Ndugu mgeni rasmi
Ndugu wanachama wote mabibi na mabwana

Awali ya yote tungeanza kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha hapa pamoja siku hii ya leo ambayo kwetu ni historia kubwa .

Ni matumaini yetu wengi wetu tumelazimika kusitisha shughuli zetu kwa siku hii ya leo kwa ajili ya jambo hili ambalo ukilitazama ni kama jambo dogo ila ukiingia kiundani zaidi ni jambo ambalo ni kubwa kuliko linavyochukuliwa .

Ikumbukwe kuwa lengo kubwa la wote kukutana hapa ni kufahamiana na kuweka mipango mikakati yatutuwezesha kuendelea kutumia vema utandawazi kupitia haya makundi ya whAssap kwa faida ya jamii na faida ya wote tuliopo katika makundi hayo.

Historia ya kundi

Kundi hili lilianzishwa na ndugu Francis Godwin ambae ni admin wa kundi hili ambalo limegawanyika katika makundi mbali mbali likiwemo kundi la Matukiodaima mchanganyiko, kundi ambalo linashughulika na matukio na mijadala mbali mbali , kundi la Siasa Kali ambalo linajumuisha viongozi mbali mbali mbali wa kiasiasa wakiwemo mawaziri ,wabunge ,viongozi wa vyama vya siasa na wapenzi na wasio kuwa wapenzi wa vyama mbali mbali za siasa lengo ni kuangazia masuala mbali mbali ya kisiasa za ndani ya nchi na nje ya nchi .

Makundi mengine ni pamoja na lile la wanahabari Tanzania ambalo limejumuisha wanahabari mbali mbali ,kundi na ndoa na urafiki ambalo limekuwa likijadili mambo ya ndoa na urafiki na hata kuwaandaa wale wanaotaka kuoa ama kutaka marafiki ili kutoa kurupuka kuingia bila kuwa na elimu na makundi mengine ambayo kwa ujumla wake ni zaidi ya makundi sita yenye malengo mbali mbali .

Hivyo kuanzishwa kwa makundi hayo kumeendelea kupanua wigo wa uelewa wa masuala mbali mbali ya kijamii kulingana na mijadala ya kila kundi na hivyo kwa sasa kila mwanachama kuweza kuelewa kwa kiasi juu ya jambo Fulani.

Kwa ujumla makundio haya yote hadi sasa toka yaanzishwe yana miezi takribani minne na kuwa na jumla ya wanachama zaidi ya 300 kati yao wanachama hai ni 60 na kati yao ni hawa waliopo hapa ukumbini leo .

Malengo ya kundi hili ni kuendelea kuelimishana juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ,pili kulifanya kundi hili kuwa kundi la kijamii ambalo litafanya kazi mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamnoja na kusaidiana na kuwasaidia watu wenye mahitaji kama yatima ,wazee,wajane na hata kusaidia kuchangia shughuli za kimaendeleo katika maeneo yetu.

Tunakusudia kulisajili kundi hili rasmi kwa kuwa na katiba yetu pamoja na kuanza kukopeshana mikopo isiyo na mashariti magumu ili kuwawezesha wanakundi kuanzisha miradi ya kiuchumi ama kuanza kujenga nyumba za kuishi na shughuli nyingine.

Kutokana na malengo hayo tumefanikiwa kuchangishana fedha kwa kila mwanachama kuchangia kulingana na uwezo wake na kupata kiasi cha Tsh milioni 1 ambazo tunazo hadi sasa kati ya kiasi cha Tsh milioni 3 ambacho tunahitaji kwa ajili ya kuanza utaratibu wa kukopeshana kwa wanachama japo 5 kwa kila mwezi mkopo wa Tsh 500,000.

Hivyo ndugu mgeni rasmi iwapo tutasaidiwa kiasi hicho cha fedha tuna uhakika tutaanza kufanya kitu ambacho jamii itaweza kuiga kutoka kwetu kupitia kundi hili la matukio daima.

Aidha tunapenda kuwashukuru wabunge na viongozi mbali mbali ambao wamweweza kuunga mkono wazo letu hata kutuchangia fedha za kufanikisha mkutano huu pamoja na wanachama wote tukliopo hapa ambao kwa uwezo wetu tumeweza kuchangishana .

Ni imani yetu kama tumeweza kuchangishana kwa siku tatu kiasi cha zaidi ya Tsjh milioni 1.5 kwa ajili ya kufanikisha mkutano huu ni matumaini yetu tunaweza kuchangishana zaidi ya milioni 10 ndani ya miezi michache na upo uwezekano wa siku kuja kuwa na taasisi yetu kamili ya kifedha .

Ndugu mgeni rasmi siku zote mpango ni kuchagua na sisi tumeamua kuchagua hili huku tukiwa na imani hata serikali yetu itatuunga mkono katika hilo na kupitia kundi hili tuna ratiba ya kuutangaza hata utaklii wa mikoa ya nyanda za juu kusini .

Changamoto ; siku zote palipo na mafanikio hapakosi changamoto hivyo changamoto kubwa ni baadhi ya wanachama kutokuwa na uwezo wa kutoa michango kwa wakati na pili kukosekana kwa miradi ya kiuchumi kwa baadhi yetu jambo linalopelekea kukwamishana katika kuchangia michango.
Kabla ya kufika mwisho tungependa tena kukushukuru wewe mgeni rasmi kwa kukubali mwaliko wetu ambao umekuja kama ghafla kwako japo tunaimani utatuunga mkono katika wazo letu hili kwa kutushika mkono. Mwisho tunakukaribisha nawe kuungana nasi na tunakuomba sasa utuzindulie kundi letu hili.

Ahsante

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...