Wednesday, 1 October 2014

Uhaba wa maji chanzo cha kusambaratika kwa ndoa






 Katibu wa CCM mkoani Iringa, Hassan Mtenga (wa pili kushoto) akisikiliza kilio cha maji kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Igunga kilichopo Ilula wilayani Kilolo, mkoa wa Iringa jana (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

Mkazi wa Ilula wilayani kilolo ambaye akifahamika jina lake mara moja akielezea tatizo la uhaba wa  maji kwa Katibu wa CCM mkoani Iringa, Hassan Mtenga (hayupo pichani) (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

Na Friday Simbaya, Kilolo

Wananchi wa mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo mkoani Iringa wamesema uhaba wa maji  ni moja ya chanzo kinachochangia kusambaratika kwa ndoa pamoja na kuongozeka kwa maambukizi ya Ukimwi, THE SCOOP imeelezwa.

 Wananchi hao wanasema kukosekana kwa huduma hiyo muhimu kunasababisha kushuka kwa uchumi wa mji huo ambao ni kati ya miji kadhaa midogo maarufu nchini.

Wakizungumza katika mkutano wa hadahra wa chama cha mapinduzi wananchi hao walisema kuwa uhaba wa maji wa muda katika mji huo umechangia kuleta migogoro katika baadhi ndoa kutokana wa wakina mama kufuata maji umbali mrefu.

 Walisema kuwa wakinamama hao wamekuwa kutumia muda mwingi kutafuta maji wakati mwingine hadi usiku ambapo wanaume na wanawake wengine hutumia mwanya huo kutongozana na kufanya ngono uzembe.

Jenima Mloza mkazi wa kijiji cha Igunga kata ya ilula alisema uhaba wa maji umekuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa kijiji hicho kutokana kutumia muda mwingi kutafuata maji kutoka kijiji cha kipaduka karibu kilometa moja.

Alisema wanalazimika kuamka asubuhi na mapema kufuata maji katika maeneo mbalimbali na kutumia muda kusubira kupata zama ya kuchota maji katika vituo vya maji vichache vilivyopo kijijini hapo ambapo dumu moja lenye uzazo wa lita 20 katika shilingi elfu moja (1000/-)na elfu mbili (3000/-).

Naye Edgar Sanga alisema shida ya maji kijijini hapo sijui itaisha lini…? Tunaiomba serikali na  sisi itukumbuke kwamba tuna haki ya kupata maji safi nasalama kama watanzania wengine maana limekuwa ni tatizo la kudumu pamoja na kwambavyanzo vya maji vipo.

Alisema kuwa maji ilula huwa yanatoka kwa mwezi mara moja na siku zingine tunalazimika kutumia  maji visima na mabondeni ambaye tunatumia kumwagilia mbogamboga na nyanya kutokana na kukosa maji salama.

Mkazi mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa kuogopa viongozi ngazi ya vijiji kuwashughulikia, alisema tatizo la maji kijijini hapo yanatoka kwa mwezi mara moja na siku zingine ambapo maji hayatoki wananunua barabara ndoo moja katika ya shilingi elfu moja na elfu mbili.

Alisema usipokuwa na hela ya kununulia maji ni lazima kutumia maji ya visima amabyo hata hivy ni ya chumvi.

“Kero hii ni ya muda mrefu, inaathiri afya zetu na shughuli za uchumi pia, tunaishi kwa kubahatisha tofauti na wananchi wengine wa baadhi ya vijiji vya mkoa huu wanaopata huduma ya maji,” alisema mwananchi hayo mbele ya Katibu wa CCM mkoani Iringa, Hassan Mtenga, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mji jana.

Taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Profesa Peter Msolla hivi karibuni inaonesha mji huo pamoja na vijiji na vitongoji vyake unahitaji zaidi ya mita za ujazo 2,500 za maji kwa siku, lakini yanayozalishwa hivi sasa ni zaidi ya mita za ujazo 800.

Profesa Msolla na Profesa Maghembe walikuwa wakihutubia wakazi wa mji huo baada ya kutemeblea mradi wa maji wa kijiji cha Vitono, Ikuka, Kipaduka na tenki la maji la Ilula Mwaya katika ziara yao ya kuelezea mikakati ya serikali ya kuboresha huduma hiyo wilayani humo. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, mji wa Ilula una wakazi wapatao 40,000.

“Kuna kero kubwa ya maji;hayatoshi kwasababu ya ongezeko kubwa la watu; miundombinu ilijengwa wakati mji huu ukiwa na watu 3,000 sasa wapo zaidi ya 40,000, maboresho yaliyofanywa ni madogo sana, tunaomba serikali iharakishe ufumbuzi wa kero hii,” alisema.

Hassan Mtenga, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, akijibu kero hizo za wananchi aliitaka Mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo wa Ilula kuhakikisha wananchi wanapata maji .

Alisema kuwa serikali imetoa shilingi bilioni 2.2 kwa ajili mradi mkubwa wa maji utafanya shida ya maji ilula itakwisha na kilichobaki sasa na serikali kutangaza ili wawekezaji wajitokeze kuwekeza kwema mradi wa maji ifikapo mwaka 2015.

Maji ni uhai na maji yana matumizi mengi katika maisha ya kila siku ya binadamu, wanyama na hata viumbe vingine hai, ikiwemo mimea.

Lakini kwa wakazi wa Mji Mdogo wa Ilula uliopo Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, upatikanaji wa maji kwao ni kitendawili cha miaka mingi sasa kwani ni tatizo sugu.
Ilula ni mji unaosifika kwa biashara mbalimbali hususan zao la nyanya na vitunguu, hali inayoufanya uwe na mkusanyiko mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wanaokwenda kwa shughuli za kilimo na biashara.

Wenyeji na wageni wanaoishi katika eneo la Nyalumbu pamoja na Ilula yenyewe wanasema tatizo la uhaba wa maji limekuwa sugu kwao ambapo huwalazimu kununua maji kwa gharama kubwa hali inayofanya uchumi wao kudorora kutokana na adha hiyo.

Adha hiyo imekuwa kero kubwa zaidi kwa wageni, hasa wafanyabiashara wanaokwenda kununua mazao huku pia hofu ya kuibuka kwa magonjwa ya milipuko kutokana na kukosekana kwa maji safi na salama ikitanda miongoni mwa wananchi wote.

Mwisho


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...