Monday, 13 October 2014

Vicent Nyerere: Kuenzi ni vitendo maneno kelele


 
 
 
 
Katika kuenzi Nyerere Day kwa vitendo Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini (CHADEMA) Vicent Nyerere, amejenga choo chenye matundu 8 katika kijiji cha Bumangi, ambapo anataraji kukabidhi kwa serikali ya kijiji mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.

Kijiji hicho ambacho kipo kata ya Muriaza Wilaya ya Butiama mkoa Wa Mara, wananchi wamekuwa wakijisaidia porini kwa muda mrefu sasa.
Nyerere alisema kuwa gharama kubwa ilitarajiwa kutumika katika ujenzi wa choo hicho lakini hadi hivi sasa, gharama inayotarajiwa kutumika ni shilingi millioni 3 kwa kuwa wanachama wa Chama Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wamejitolea kufanya kibarua bila malipo.

"Tumejenga Choo kijiji jirani cha Bumangi soko ili wananchi wapate kujisaidia kuliko kwenda porini," alisema Nyerere.

 Aliongeza kuwa soko la bumangi hufanyika Mara moja kwa wiki na linahudumia zaidi ya vijijini 37 hivyo wananchi hukumbana na adha kubwa kwa kujisaisaidia porini kutokana na kutokuwa na choo.

Nyerere ametoa wito kwa wakazi wa maeneo ya Bumangi kutumia choo hicho kwa usafi na kukitunza ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.

Alisema Maliwato/choo ni sehemu muhimu sana katika eneo lolote linalotumiwa na binadamu na ni sehemu inayohitaji usafi wa hali ya juu sana ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...