Wednesday, 26 November 2014

MRADI WA KUWAWEZESHA AKINA MAMA KATIKA KILIMO PAWAGA


Mwakilishi wa ubalozi wa marekani David Feldmann akihutubia mamia ya wakazi wa vijiji vya tarafa ya Pawaga wakati sherehe ya kufunga mafunzo ya mradi wa kuwawezesha akina katika kilimo kupitia asasi ya mpango salama wa maendeleo ya vijana (SYDS) kwa ufadhili ya watu wa marekani.  Alisema kuwa kilimo bora ni kile chenye kuleta tija na mafanikio.

Jumla ya vikundi 43 vya wajasiliamali ambao ni sawasawa na wanawake na vijana zaidi ya 300  wa tarafa ya Pawaga wilayani Iringa, mkoa wa Iringa wamenufaika na mafunzo ya kuwezesha akina mama katika kilimo kutoka SYDS.
Mafunzo hayo yaliendeshwa na asasi isiyo ya kiserikali ya mpango salama wa maendeleo ya vijana (SYDS) kwa ufadhili wa serikali ya marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati sherehe ya kufunga mradi huo wa mrejesho kwa vikundi, meneja mahusiano wa SYDS, Arnold Pangani alisema SYDS imejitoa  kuendeleza mapambano dhidi ya changamoto zinazowakabili wengi wa akina mama katika sekta kilimo nchini.
Alisema kuwa SYDS ilienda mbali zaidi na kubaini kuwa sehemu kubwa ya wanawake wamekuwa wakijishughulisha na  katika kilimo huku wakikabiliana na changamoto lukuki kiasi cha kutofanyikwa kwa kiwango stahiki.
Alisema kuwa kilimo bora ni kile chenye kuleta tija na mafanikio na kuongeza kuwa ni jukumu la kila mwananchi wa Pawaga kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika kuinua  na kukuza uchumi wa familia  kwa kufuata mpango salama wa kilimo bora bila kujali tofauti ya kijinsia.
“SDYS kwa udhamini wa serikali ya Marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania tunaungana kwa pamoja na wananchi wa Pawaga zaidi tukitambua ushiriki wa wanawake katika kilimo,” alisema Panagani.
Aidha, wanavikundi walitoa shukrani ya dhati kwa SDYS kwa kuwapatia mwongozo bora ambao umewawezesha kupata uelewa juu ya elimu ya mpango biashara na uendashaji vikundi.
Walisema kuwa kuja kwa asasi ya SDYS kumeweza kuhamasika na kuunda vikundi ambavyo vitasaidia katika shughulu za kilimo.
Walisema kwa mafunzo hayo kama vijana wametambua umuhimu wao kama vijana ni nguvu kazi na wanatakiwa kushiriki  shughuli za maendeleo na kujifunza zaidi juu ya mpango salama kwa maendeleo ya vijana.
Kwa upande wake mwakilishi wa ubalozi wa marekani nchini Tanzania, David S. Feldmann alisema Tanzania itajengwa na watazania wenyewe na marekani itajengwa na wamarekani.
Alisema kuwa matatizo ya watanzania hayawezi kumalizwa na marekani isipokuwa katika uwezekaji ndiyo suluhisho matatizo yote.
Alisema ni jukumu kwa kila mwananchi kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika kuinua na kukuza uchumi.

Alisema watanzania lazima walipe kodi kwa serikali iliwaweze kupatiwa huduma stahiki kutoa kwa serikali kama ilivyo marekani.
Alisema kuwa asilimia 90 ya serikali ya marekani inaendeshwa kwa mapato ya ndani kwa vile wananchi wengi wanalipa kodi kwa serikali bila kutegemea misaada ya nje.

















No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...