Sunday, 2 November 2014

NEEMA CRAFTS WATOA MSAADA WA BASKELI KWA WALEMAVU

Walemavu Mkoani Iringa wakifurahia baada ya kukabidhiwa baskeli zao ikiwa ni msaada kutoka Neema Crafts

Mkurugenzi Mtendaji wa Neema Crafts Bwana Benjamin Ray akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa baskeli walioutoa kwa walemavu wa Mkoani Iringa. 



Na Simon Victor

Walemavu mbalimbali mkoani Iringa hapo jana walipewa msaada wa baskeli arobaini (40) kutoka Neema Crafts ambao wako chini ya dayosisi ya Ruaha.

Mkurugenzi mtendaji wa Neema Crafts bwana Benjamin Ray akizungumza kwenye makabidhiano hayo alisema kuwa, Neema crafts ilianzishwa mwaka 2003 chini ya dayosisi ya Ruaha.


Ilianza ikiwa na viziwi watatu na walikuwa wakijishungulisha na utengenezaji wa karatasi. Mwaka 2009 walijenga jengo ambalo wanalitumia kwa mgahawa na mwaka 2011 waliongeza jengo jingine ambalo wanitumia kama nyumba ya kulala wageni ambayo inasimamiwa na walemavu na kuwa nyumba ya kwanza ya kulala wageni kusimamiwa na walemavu wa kuongea(Mabubu).

Bwana Ray alisema miradi yao yote inasimamiwa na walemavu wa aina mbali mbali. Pia Ray isema msaada wa baskeli waliotoa kwa walemavu ni zawadi waliyopewa kutoka nchini Marekani katika jimbo la Minnesota.

Nae Mwenyekiti wa Walemavu(CHAWATA) mkoani Iringa Bw. Shaabani Shomari aliwashukuru Neema Crafts kwa msaada waliotoa kwao.Lakini akatatoa angalizo kwa walemavu wote waliopata baskeli hizo wazitumie kwa madhumuni yaliokusudiwa.

Pia Katibu wa CHAWATA Mkoa wa Iringa, Haruna Mbata amewapongeza Neema Crafts kwa kuwa bega kwa bega na wao na msaada waliotoa ni chachu kwa maendeleo ya walemavu mkoani Iringa. (CHANZO MJENGWABLOG)

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...