Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Dkt Christine Ishengoma (wa pili kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya
Iringa, Leticia Warioba jana kabla ya kukabidhi msaada wa mifuko 115 ya sementi
yenye thamani 1,725,000/- kwa ajili ya
ujenzi wa maabara katika shule za sekondari. Wanaoshuhidia ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Iringa, Ayub Wamoja (kulia) na mkurugenzi wa Manispaa ya
Iringa, Theresia Mahongo. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt
Christine Ishengoma jana amekabidhi msaada wa mifuko 115 ya sementi yenye
thamani 1,725,000/-kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo kwa
ajili ya ujenzi wa maabara katika shule
za sekondari.
Dkt. Ishengoma kwa kupitia
ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa ametoa mifuko ya sementi hiyo ili kutekeleza agizo la Rais
Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara na kuwataka wananchi na taasisi mbalimbali
kujitolea kuchangia ujenzi huo ili kuongeza kasi ya kuzalisha walimu wa masomo
ya sayansi.
Alisema kuwa ujenzi wa
maabara katika shule za sekondari ni utekelezaji wa agizo la rais aliyezitaka
shule zote za sekondari nchini kuwa na maabara tatu kwa kila shule.
Akipokea msaada huo wa
vifaa vya ujenzi mkuu wa wilaya iringa, Leticia Warioba kwa niaba Mkurugenzi wa
Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo aliwaomba wadau mbalimbali yakiwemo mashirika,
taasisi, watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kujitokeza kuchangia ujenzi wa
maabara.
Warioba alisema kuwa ili
kufanikisha malengo ya wilaya ya iringa inahitaji michango ya wadau mbalimbali ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete
aliyezitaka halmashauri zote kuhakikisha zinajenga maabara katika shule
za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo alisema manispaa hiyo inahitaji maabara za kudumu 28 na hadi sasa kuna jumla ya maabara 22 zinaendelea kujengwa na maabara sita ziko katika hatua ya mwisho kukamilika.
Hata hivyo, maabara
zinazoendelea kujengwa katika manispaa hiyo ni pamoja na vyumba vya maabara ya
fizikia, kemia na baiolojia ifikapo mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment