Ofisa Elimu Mkoa wa Iringa, Joseph Mnyikambi akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwaka. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Na Friday Simbaya,
Iringa
MITIHANI ya wanafunzi wa
kidato cha nne na maarifa (Qualifying Test) kitaifa unatarajia kufanya nchini
kote hapo tarehe 3 Novemba mwaka huu.
Mkoa wa Iringa unatarajia
kuwa na jumla ya watahiniwa 11,781 watakaofanya mtihani wa kidato cha nne na
mtihani wa QT taifa na kuaswa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ambavyo vitakavyowaondolea
sifa ya kuendelea kufanya mitihani yao.
Rai hiyo imetolewa na Ofisa
Elimu Mkoa wa Iringa, Joseph Mnyikambi jana wakati akiongea na waandishi
wa habari ofisini kwake.
Ofisa Elimu wa Mkoa wa
Iringa alisema kuwa watahiniwa wanatakiwa kujiepusha na vitendo vyote vya udanganyifu
ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye vyumba vya mitihani na karatasi za majibu na
kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutawaondolea sifa ya kuendelea mitihani yao.
“Nikiwa kama ofisa elimu
mkoa wa Iringa nimeagiza watahiniwa wote kuzingatia maelekezo ya wasimamizi wa
mitihani na wasimamizi nao wazigantie maelekezo ya semina ya maelekezo kwa
wasimamizi,” alisema ofisa huyo.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa
utakuwa na jumla ya vituo vya kufanyia mitihani 186 na vitasimamiwa na wasimamizi
408 ambapo, wasimamizi wakuu watakuwa 46 pamoja na walimu 309 watakaosimamia mitihani ya vitendo (practical
tests).
Aidha, ofisa huyo alisema
kuwa kwa mwaka jana Mkoa wa Iringa ulivuka lengo la ufaulu ya matokeo makubwa
sasa (BRN) ya asilimia 60 kwa kufaulisha wanafunzi zaidi kwa asimilia 64.92 na
kuongeza kuwa mwaka lengo ni asilimia 70.
Hivyo aliwataka
watahiniwa wote wanaotarajia kufanya mitihani hiyo, kujiamini kwa vile katika
kipindi cha muda wa miaka minne waliyokuwa shuleni wamejifunza mambo yote ya
msingi watakayofanyia mihitani hiyo.
No comments:
Post a Comment