Tuesday, 4 November 2014

Watu wawili wamefariki dunia mkoani Iringa



Watu wawili wamefariki dunia mkoani Iringa katika matukio tofauti ikiwapo la mkazi wa Kijiji cha Bumilayinga Kata ya Bumilayinga tarafa ya Malangali wilayani Mufindi kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali.

Akingumza na waandishi wa habari ofisni kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema kuwa Maurisia Malangalila (65) aliuawa kwa kukatwa shingo na kitu chenye ncha kali na Patrick Ngelenge.

Alisema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 01.11.2014 majira ya saa 21:00 hrs karibu na nyumba aliyokuwa akiishi marehemu ambapo aliuawa kwa kukatwa shingo na kitu chenye ncha kali.

"Mwili wa marehemu ulikutwa barabarani jirani na nyumba na mtuhumiwa ametoloka baada ya kufanya tukio hilo," alielezea.

Katika tukio la lingine Kamanda Mungi alisema huko katika Kijiji cha Ifunda, Tarafa ya Kiponzero wilayani Iringa, mkoani Iringa Pogras Mage, 36 aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichani na watu wasiofahamika.

Alisema kuwa marehemu Mage aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika.

Tukio hilo lilitokea tarehe 01.11.2014 majira ya saa 22:00 hrs katika kijiji cha Ifundi tarafa ya kiponzero wilaya ya Iringa vijijini.

Aidha Mungi ametoa rai kwa jamii kutojichukulia sheria mkoanoni na badala yake kuwanautaratibu wa kuwashitaki kisheria kabla ya kuchukua hatua ya kupiga hadi kupelekea kuua.

Hata hivyo, katika matukio yote mawili watuhumiwa hawajakamatwa na chanzo cha matukio kinachunguzwa

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...