Katibu Mkuu wa TUPSE, Edison Kivelege akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Baadhi wa walinzi wakiwa mabegi ofisini kwa TUPSE
ZAIDI
ya walinzi 60 wa Kampuni ya Kiwango Security Guards Ltd kanda ya Iringa kwa
mara nyingine wamegoma kuendelea na kazi ya kulinda minara ya Vodacom/Tigo wakidai
mishahara ya miezi mitatu.
Walinzi
hao kutoka sehemu mbalimbali ya mkoa wa Iringa wakiongea na SIMBAYABLOG leo kwa machungu katika
ofisi za Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE), Kanda Nyanda
za juu Kusini zilizopo mjini Iringa, walisema kuwa wana muomba Rais Jakaya Kikwete
aingilie kati katika mgogoro wa mwajiri wao ili awalipe mishahara yao ya miezi
mitatu wanayomdai.
"Mwajiri
huyo ni wa kampuni ya ulinzi ya kiwango kutoka jijini Dar es salaam hajatulipa
mishahara yetu, kwa kweli hali ni nguu kweli sasa sisi tunafanya kazi kama
nyuki tunatumikishwa na hadi sasa tuna miezi mitatu na zaidi hatujalipwa na hatujui
familia zetu zinaishi vipi huko nyuma, hivyo tunamuomba rais aingilie kati
suala hili ilituwezekulipwa mishahara yetu.'walisema.
Mzee
Ismaili Mpenge (68) ambaye analinda mnara wa Vodacom kadeti uliopo kijiji cha
Nyang'oro katika jimbo la isimani Iringa alisema kampuni hiyo haijamlipa
mishahara ya miezi miwili tangu aanze kazi Julai nne mwaka huu.
Alisema
kuwa tangu jana afike mjini iringa kutoka kijijini kwake hajala na nauli
yakufika mjini amekopa na kuongeza kuwa hapa mjini hana ndugu na kuomba wasamaria
wema wamsaidie sehemu ya kulala anaposubiria malipo.
"Nimetoka
katika kijiji cha Nyang'oro tangu jana na sijui hatma na isitoshe tuna watoto
wanasoma na mpaka sasa hatujui familia zetu zinakula nini mpaka sasa ... kwa
kweli maisha yetu walinzi ni magumu," alisema.
Naye
Isaya Mdabagi mlinzi wa mnara wa migori alisema kuwa kwa miezi miwili
hatujalipwa mishahara ukizingatia tuna familia tulizoziacha huku nyumbani bila
chochote.
Mwajiri
aliahidi kulipa mshahara wa mwezi moja na sio mshahara wote kama makubaliano
yetu ya kulipwa laki na ishirini lakini amesema kuwa watalipwa shilingi elfu
themanini .
Hata
hivyo, kuna baadhi ya walinzi ambao waliokosa hela ya kulala gesti waliamua kulala ofisiza TUPSE
kwa kukosa ndugu hapa mjini.
Kwa
Upande wake Katibu Mkuu wa TUPSE, Edison Kivelege aliongeza kuwa Iringa ina
jumla ya makampuni ya ulinzi binafsi 36 nyingi zikitoka nje ya mkoa, lakini
pamoja na hayo kampuni zenye ofisi azizidi kumi (10) na kusababisha kukosa
mawasiliano.
Alisema
kuwa chama kinapotaka kuwasiliana na wanachama wake kinapata shida ya kuonana
na viongozi kwa ajili yakutatua kero za wanachama kwa sababu ofisi nyingi za
waajiri zipo Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam.
Alisema
kuwa kampuni nyingi hapa Iringa zinafanyakazi za udalali kwa sababu hiyo
kampuni hizo zinakuwa zinawaajiri walinzi wasiokidhi vigezo ambao wanakuwa na
uweledi mdogo kuhusiana na masuala ya ulinzi na wengine kuajiriwa bila mikataba
maalum.
Katibu
Mkuu wa TUPSE huyo aliwaasa walinzi kuacha tabia ya kuhamahama makampuni kwa
sababu wanajisababishia kupoteza mafao na uaminifu na kuwahimiza wajisajili na
chama hicho ili washiriki katika mabaraza ya majadiliano na waajiri.
No comments:
Post a Comment