Tuesday, 23 December 2014

BOMA LA MJERUMANI KUJENGWA MAKUMBUMSHO YA KISASA

CHUO Kikuu cha Iringa (UOI) kupitia mradi wa kuendeleza utamaduni nyanda za juu kusini uitwao Fahari Yetu (Southern Highlands Culture Solutions) kinatarajia kuanza ukarabati wa jingo la kale lilojengwa na serikali ya Ujerumani enzi za ukoloni 'Boma' mkoani Iringa.


Mradi huu wa kitalii ambao ni wa mamilioni ya shilingi za kitanzania utahusisha ukarabati, uhifadhi na uhuishaji wa iliyokuwa boma ya Iringa enzi za utawala wa kijerumani.


Akizungumza na waandishi wa habari jana naibu makamu mkuu wa chuo Dr. Hosea Mpogole kwa niaba ya kikuu cha Iringa zamani Chuo Kikuu cha Tumaini Profesa Nicholas Bangu alisema makubumsho ni kati ya maeneo bora kabisa duniani ya kujifunzia, kufanya maonyesho ya mambo ya kisayansi kama uvumbuzi, kazi za sanaa na za kihistoria na pia ni kituo muhimu kwa ajili ya utafiti, matamasha ya asili na ushawishi.


Alisema kwamba chuo kikuu cha Iringa kimejikita katika kutoa uwezo wa kitaaluma ambao utatoa fursa ya kufundisha kwa vitendo badala ya kuwa na nadharia pekee.


"Mradi huu wa Fahari Yetu umetenga fedha kwa ajili ya ukarabati ambao pia itaibadilisha Boma hili na kulifanya kuwa jingo la makumbusho ya urithi wa kiutamaduni. Mradi huu makao makuu yake yatakuwa chuo kikuu cha Iringa utafanya kazi kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii idara ya mambo ya kale, makumbumsho ya taifa, na ofisi ya mkuu wa mkoa Iringa ambao wote ni wadau wa Fahari Yetu," alisema Dr. Mpogole.


Dr. Mpogole pia alisema chuo kinapitia upya na kuboresha mtaala wake wa idara ya utamaduni na utalii (Cultural Anthropology and Tourism) ili kuboresha kozi hiyo na utafiti katika kuhakikisha kuwa taaluma inaunganisha shughuli za urithi wa mambo ya asili, utamaduni na uhifadhi kwa ajili ya kukuza sekta ya utalii nyanda za juu kusini na taifa kwa ujumla.


Dr. Mpogole aliongeza kuwa jengo la makumbumsho hilo ambalo hapo awali lilikuwa ni ofisi ya mkuu wa wilaya Iringa, litaleta manufaa katika kukuza na kuendeleza sekta za wajasiliamali wadogowadogo ambao moja kwa moja watahusiana na utalii wa kitamaduni.


Naye Katibu wa tawala wa mkoa wa Iringa, Ayub Wamoja kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Juma Masenza alisema kuwepokwa makumbumsho ndani ya mkoa kutakuza kwa kiwango kikubwa sekta ya utalii ndani ya nchi kwa kuongeza thamani ya vivutio.


Na pia kuwafanya watalii kukaa muda mrefu ndani ya nchi na hatimaye kuliongezea taifa pato.


Alisema matokeo la ongezeka la watalii ni pia ongozeko la ajira kwa mtu mmoja mmoja na hata sekta mbalimbali zinazojishughulisha na utalii hasa pale wajasilamali watakapoona fursa za uwekezaji katika tasnia ya utalii na utamaduni.


Katibu tawala huyo alisema kuwa nyanda za juu kusini zimebarikiwa kuwa na urithi mkubwa wa mali asili na utamaduni, hata hivyo bado urithi huu hajatumika ipasavyo ili kuweza kuchangia katika kukuza maisha ya jamii kutokana na ukosefu wa ufahamu bora miongoni mwa mwanajamii juu ya umhimu wa urithi wa utamaduni.


Alisema jengo hilo la kisasa la makumbumsho litakuwa katika iliyokuwa Iringa boma, jengo ambalo lilinjengwa na na utawala wa kikoloni wa kijerumani litatumika kwa ajili ya kuonesha mambo ya urithi wa kihistoria na kuvitia watalii duniani kote kuja kutembelea mkoa wa Iringa na vivutio vyake.


Hata hivyo ofisi ya mkuu wa mkoa, halmashauri ya Iringa, Manispaa ya Iringa, Makumbusho ya taifa, na Chuo Kikuu cha Iringa ndio washirika wakuu wa mradi wa Fahari Yetu-Southern Highlands Cultural Solutions kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU).

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...