Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Simanjiro,Ambrose Ndege.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Simanjiro, Ambrose Ndege, amedai kuwapo mbinu chafu zinazofanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwawekea pingamizi wagombea wa chama chake wa nafasi za wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.
Alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akiwatambulisha wagombea 24 wanaotarajia kugombea nafasi hizo kwenye Mji Mdogo wa Mirerani, katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.
“Haiwezekani chama hicho chenye wagombea makini kuliko CCM waondolewe kwa kinachodaiwa kukosea kujaza fomu ilhali CCM yenye wagombea dhaifu na wasio na elimu kubwa waweze kujaza fomu hizo,” alisema Ndege
Aliongeza: “Kuna mbinu chafu zimetumika ikiwemo rushwa, kuwaengua wagombea wetu ili CCM wapite jambo ambalo hatuwezi kulikubali hata mahakamani kudai haki yetu.”
Alisema watapigania kudai haki yao ili kuhakikisha wagombea uenyekiti wa vitongoji waliowekewa pingamizi wanarudishwa.
Wagombea wote 12 wa Kata ya Endiamtu walioondolewa ni Zephania Mungaya (Mji mpya), Saimon Mwakyusa (Sekondari) alijidhamini mwenyewe na kuandika kijiji cha Endiamtu ilhali kata hiyo haina vijiji. Ina vitongoji.
Wengine ni Maboni Kajia (Tupendane), Nicktemas Mollel (Zaire), David Kyara (Kazamoyo), Philemon Oyogo (Kazamoyo Juu), Zakayo Emmanuel (Kisimani), Alfred Mushi (Endiamtu), Basil Sichambaga (Tanesco), Godson Akia (Tanki la maji), Thiphon Costantine (Kilimahewa) na Tikisael Nyari (Kairo).
Kwenye Kata ya Mirerani, wagombea wanne wa Chadema wameondolewa kwenye kinyang’anyiro na kubaki wanane, huku Christopher Chengula (Tunduru) akishinda pingamizi lililowekwa na wana CCM kuwa siyo mkazi wa eneo hilo.
Walioondolewa Kata ya Mirerani, ni Dickson Kafarans aliyeomba Kitongoji cha Songambele B kisichokuwapo, Evarest Shirima aliomba Machinjioni kisichokuwapo, Stanley Stephen (Kangaroo) siyo mkazi na Godfrey James (Songambele) alihamia wiki moja iliyopita.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment