Enock Sontonga
JE, unamfahamu mtu aliyetunga sauti (melody ) ya wimbo ambao leo Watanzania wanauita Wimbo wa Taifa?
Huyu ni Enock Sontonga, raia wa Afrika Kusini, aliyetunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ iAfrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905.
Sauti ya wimbo huo imetumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini zimetunga nyimbo nyingine.
Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897 na kurekebishwa na wahariri mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa.
No comments:
Post a Comment