Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dkt. Leticia Warioba (katikati) akipata maelezo namna ya kujiunga na vifurushi wa king'amuzi cha StarTimes kutoka kwa afisa habari na masoko, Erick Cyprian huku meneja wa tawi la StarTimes mkoa wa iringa Boki Shabani wakati uzinduzi wa duka hilo
leo.
Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi mlangali, manispaa ya Iringa, Grace Nyimbi akifurahia zawadi ya kalama kwa kujaribu kuandika wakati uzinduzi wa duka hilo leo.
Mkaguzi msadizi wa wilaya, Ibrahim D.RC akipekea zawadi ya kisimbuzi kwa ya OCD Iringa kutoka meneja wa tawi la startimes mkoa wa iringa, Boki Shabani wakati uzinduzi wa duka hilo leo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba akipekea zawadi ya
kisimbuzi huku meneja wa tawi la startimes mkoa wa iringa, Boki
Shabani akishuhudia wakati uzinduzi wa duka hilo leo. (PICHA ZOTE NA
FRIDAYSIMBAYA)
Katika kuhakikisha watanzania wanafikiwa na matangazo
ya uhakika ya digitali, kampuni ya startimes imezindua duka kwa ajili yakutolea
huduma za madishi (DTH) katika mkoa wa Iringa.
Kufunguliwa kwa huduma za kampuni hiyo mkoani iringa
kunafanya idadi ya matawi nchi nzima kufikia 15 huku sehemu nyingine zikiwa
mbioni kufunguliwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hili jipya, Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia warioba alipongeza jitihada za dhati za
kampunihiyokwa kuyaleta matangazoya digitali wilayani kwake kwani kilikuwa ni
kilio kikubwa cha wananchi wake na ana imani kuwa fursa hiyo itatumika kuinua
shughuli za kiuchumi.
“Hakuna asiyefahamu umuhumuwamatangazo ya televisheni nchini,kutazama
televisheni sio kitu cha anasa kama ilivyokuwa ikitafasiriwa kipindi cha nyuma.
Kupitia matangazo hayo wananchi wanaweza kutafuta taarifa mbalimbali za habari,
maendeleo ya kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia,”Dkt. Warioba alisema.
“Wakulima nawaombaa mtumie kutazama vipindi vinavyohusu
kilimo,kupata taarifa za pembejeo na masoko. Wafanyabiashara tumieni fursa hii
kuweza kujua maeneo sahihi ya kuwekeza, kuuza bidhaa zenu na pia kujua
wafanyabiashara wenzenu sehumu nyingine. Hivyo hata wanafunzi nao
watazamevipindi ambavyo vitawaongezea maarifa na ujuzi zaidi na kuweza kufaulu
katika masomo yao,” aliongeza Dkt. Warioba.
Aidha mkuu wa wilaya ya Iringa huyo amewataka wananchi
wake kuyapokea mabadiliko hayo mapya ya sayansi na tekinolojia kwa dunia nzima
inabadilika na wao hawanabudi kufanya hivyo.
Alisemakuwa imekuwa kawaida kwa wananchi
wengikulalamika linapokuja suala la kupokea mfumo mpya wa maisha, na kuongeza
kuwa ‘information is power’ kwa lugha ya Kiswahili habari ni nguvu.
Aliwaasa wanairnga kutofanya hivyo bali wapokee kwa
nguvu moja mabadiliko hayo wakiamini yatasogeza mbele zaidi maendeleo yao.
Kwa upande wake meneja wa duka hilo jipya mkoani
Iringa, Boki Shabani alibainisha kuwa kuzinduliwa rasmi kwa huduma zao mkoani
hapa ni jitihada za dhati kabisa za startimie kuhakikisha inwafikia watanzania
popote pale walipo.
Alisema kuwa ni dhahiri kuwa dunia sas inakimbilia
kufikia n2015 ambao ndio mwisho wa kutumia masafa ya analojia na kwa umakini wa
serikali ya Tanzania imeamua kuanza mapema mchakato huu tangu 2010.
Ambapo mwaka 2012 mikoa mbalimbali ilizimwa kama Dar es
Salaam, Dodoma, Arusha, Mbeya na Moshi na sasa mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment