Leo Kundi la WAZO HURU limejumuika na kutembelea watoto yatima na wenye maisha magumu
wanaoishi katika kituo kilichopo Kijiji cha Tosamaganga, Kata ya Kalenga,
Wilaya ya Iringa vijijini ambapo kituo hicho kina jumla ya watoto 80 ambapo
kati yao watoto 15 ni wachanga kabisa kuanzia siku moja hadi miezi minne.
Wote walioshiriki jambo hili ni watu ambao wapo kwenye
kundi la Watsup linaloitwa WAZO HURU ambapo Mwenyekiti wa kundi hili, Mathias Canal kwa pamoja
walikamilisha adhma yao hii ambayo tuliianza muda mrefu.
Kituo hiki kilianza mwaka 1969, ambapo miaka minne
iliyopita serikali ilichangia shilingi milioni 5 lakini hadi hivi sasa bado
kituo kinahitaji misaada ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kusoma.
Kituo hiki kinasimamiwa na masista wa Teresina na
kinasimamiwa na Sista Helena Kihwele katika kijiji cha Tosamaganga jimbo ya
Iringa.
Kikundi cha wazo huru pamoja na mambo mengine walitoa
msaada wa sukuri, mchele, sabuni na unga wa ngano.
No comments:
Post a Comment