Thursday, 12 February 2015

DC MUFINDI APANDISHWA KIZIMBANI


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo Februari 12, inampandisha kizimbani Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evalista Kalulu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya Sh Milioni 3, fedha za umma.

Pamoja na mkuu huyo wa wilaya wapo watumishi wengine wanne wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wake wa halmashauri, Limbakisye Shimwela.

Kwasasa Limbakiyse Shimwela ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Taarifa za uhakika zilizothibitishwa na DC Kalalu kwa njia ya simu alipokuwa akiongea na mtandao huu mapema hii leo zinaonesha fedha hizo zilichangwa na wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wilaya hiyo.

“Ni kweli, mimi na wengine wanne tunatuhumiwa kutumia kiasi hicho cha fedha vibaya. Fedha hizo zilichangwa na wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo,” alisema.

Alisema wamepata tuhuma hiyo kwa kile kinachoelezwa kwamba zilitumika bila kufuata taratibu za zabuni.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...