Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa (Chadema) hayupo pichani akihutubia wakazi wa Kihesa jana katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya kihesa sokoni. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Mbunge wa
Jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa (Chadema) ameahidi kutoa maji ya kunywa mji mzima kwa wananchi endapo litatokea
jua kali wakati wa kujiandikisha katika
daftari la mpigakura litakapofika Manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa
ofisi ya mbunge ipo tayari kutoa maji ya
kunywa kwa mji mzima kwa wananchi watakaojitokeza kujiandikisha katika daftari
la mpigakura wakiwa katika foleni , wakati wakujiandikisha pindi daftari
litakapo wasili Manispaa ya Iringa.
Mch. Msigwa
aliyasema hayo jana wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika katika viwanja
vya Kihesa sokoni wa kuzindua ziara ya siku kumi na nane (18) ya baraza la
vijana chadema (BAVICHA) mjini Iringa yakupita kila kata kuhamasisha vijana
kujiunga na chama hicho pamoja na kupata vijana 200 watakaojiunga Red Bridged.
Alisema kuwa vijana hao 200 kila kata watakaojiunga
katika vikundi vya ulinzi na usalama wa chama hicho watapatiwa mafunzo
yaukakamavu kwa ajili ya afya na hamasa kwa lengo la kulinda viongozi wa chama
pamoja na mali zake.
Alisema kuwa
kuna watu wanadai kwamba vikundi vya vijana vya ulinzi na usalama yaani ‘red brigade’
vipo kwa ajili yakufanya ugaidi kama baadhi ya watu wanavyodai, kumbe vikundi
hivyo kwa ajili ya ulinzi wa viongozi wa chama pamoja na kulinda kura zisiibiwe
wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu.
Alisema kuwa
lengo ya ziara hiyo BAVICHA nikupata vijana 3,600 wakujitolea watakaojiunga na
red brigade kwa ajili kupewa mafunzo ya ukakamavu kwa lengo ya kuwapatia afya
na hamasa.
Aliongeza kuwa
lengo lingine ya ziara ni pamoja na kuhamasisha watu wajiunge na chama ili
kujenga chama na wajitokeze kwa wingi wakati daftari la mpigakura litakapofika
Manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa
kama watu wanataka kuiondoa serikali ya CCM madarakani basi, hawanabudi
kujitokeza kwa wingi kujiandisha katika daftari la kudumu la mpigakura litakapo
wasili mkoani Iringa, kwa sababu bila kuwa na kadi ya mpigakura hawataruhusiwa
kupiga kura.
Pia, Mch.
Msigwa alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa mji wa Makambako, mkoani
Njombe kwa kuonyesha mfano mzuri kwa kujiandikisha kwa wingi ambapo walivuka
lengo la tume ya uchaguzi (NEC) la kuta kuandikisha wapiga kura 32,000 na
badala yake walijiandikishwa wapigakura
47,000.
“Wananchi wa
kule Makambako wamenifurahisha sana kwa kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha
kwa fujo, hii inaonesha jinsi gani watu walivyokuwa na mwamko mkubwa wakutaka
mabadiliko,” alisema Mch. Msigwa.
Alisema kuwa
hivi sasa moto wa UKAWA ni mkubwa sana wakutaka kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
madarakani.
Aliongeza kuwa
watu wanatakiwa kujitokeza kujiandikisha ili kuweza kuipatia Chadema
halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kuwapigia kura viongozi wa Chadema
watakaosimamishwa kugombea viti vya udiwani wakati Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka
huu.
Alisema kuwa
kuipatia Chadema halmashauri itakuwa na uwezo wa kubadilisha taswira ya
Manispaa ya Iringa kuliko ilivyo sasa kwa kuwa
itakuwa na mahusiano na miji mingine nje ya nchi kwa ajili kubadilishana
uzoefu.
Kwa upande
wa utalii, alisema kuwa sekta ya utalii nchini haijaboreshwa na kuwekewa miundombinu
mizuri kuweza kukuza uchumi na kuaajiri watu wengi zaidi kupitia shughuli za
kitalii.
Alitoa mfano
wa Uwanja wa Ndege wa Nduli uliopo mjini Iringa kuwa kuboreshwa vizuri ndege
kubwa zitatua na kuleta watalii wengi zaidi kutembelea vivutio ambavyo vipo
mkoani hapa na hatimaye kukuza utalii ukanda wa kusini (southern circuit).
Alisema kuwa
idadi ya watalii ikiwa kubwa hapa watanunua vinyago kwa wauza vinyago, watalala
katika mahoteli, madereva taxi nao watafanya biashara ya kusafirisha watalii
kwenda maeneo mbalimbali ya mkoa kuangalia vivutio vya utalii na hatimaye
mzunguko wa pesa utakuwa mkubwa.
alisema kuwa
mzunguko wa pesa ukiwa mkubwa watu watafanya biashara hata yule muuza mboga
atanufaika pia na hatimaye kuboresha maisha yao.
Alisema kwa
sasa Tanzania haina hoteli nyingi za nyota tano (Five Star hotels) kwa mfano,
wakifika watalii 500 hakuna mahali watakapolala kwa kukosa hoteli zenye hadhi
hiyo, hivyo tunahitaji ujenzi wa hoteli nyingi zenye hadhi.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa BAVICHA mjini Iringa, Leonce Marto alisema kuwa lengo ya
ziara katika ujenzi wa chama pamoja na kuunda mabaraza ya vijana kila kata kwa
ajili ya hamasa.
Alisema kuwa
wanahitaji vijana 3,600 kutoka katika kata 18 za Manispaa ya Iringa,kila kata
wapatikane vjiana 200 ambao watapatiwa mafunzo ya ukakamavu kwa ajili ya afya
na hamasa.
Alisema kuwa kazi nyingine ya ziara ni
kuhamasisha watu vijana kwa wazee wajitokeze kujiandikisha katika daftari la kudumu
la mpigakura ili kuwaandaa kisaikolojia pindi daftari litakapofika Manispaa ya
Iringa.
Alisema kuwa
katika ziara hiyo watahamasisha vijana waliofikisha umri wa miaka 18 na
kuendelea kujiaandikisha katika daftari ya mpigakura wakiwemo kina mama kwa
sababu wao ni kiini cha mabadiliko.
No comments:
Post a Comment