Mwenyekiti mtendaji wa taasisi ya maendeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA), Charles Nchimbi (kushoto mwenye kapelo) akifuatilia ushiriki wa wawashiriki wa wanasemina wa kutoka chama cha viziwi mkoani Iringa wakati meneja uhusiano kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji (CMSA) Charles Shirima (hayupo picha) akitoa mada ya dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji kwa chama cha viziwi tanzania jana. (Picha na Friday Simbaya)
Washiriki kutoka chama cha viziwi mkoani Iringa wakifuatilia semina ya mafunzo kwa umakini kuhusu dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji jana iliyoandaliwa na mamlaka ya mitaji na dhamana (CMSA) kwa kushirikiana na taasisi ya maenedeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA) hapa mkoani Iringa. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima akitoa mada wakati wa semina ya mafunzo kwa chama cha viziwi Tanzania kuhusu dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji jana iliyoandaliwa na mamlaka ya mitaji na dhamana (CMSA) kwa kushirikiana na taasisi ya maenedeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA) hapa mkoani Iringa. Kulia ni mkalimani lugha ya alama. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Meneja Uendelezaji wa Masoko ya Mitaji (CMSA), Nicodemus Mkama akitoa mada wakati wa semina ya mafunzo kwa chama cha viziwi Tanzania kuhusu dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji jana iliyoandaliwa na mamlaka ya mitaji na dhamana (CMSA) kwa kushirikiana na taasisi ya maenedeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA) hapa mkoani Iringa. Kulia ni mkalimani lugha ya alama. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
MKUU wa Mkoa wa Iringa,
Amina Masenza amewaasa wananchi kuepuka kukimbilia uwekezaji wa kutengeneza
hela nyingi kwa haraka.
Alisema hali hiyo huwa
inasababisha watu wengi kutapeliwa fedha zao na kujiingiza kwenye biashara na
uwekezaji usio halali na mara nyingine kujikuta wanavunja sheria na kujiunga na
michezo ya upatu haramu na kupoteza fedha zao.
Masenza alitoa kauli
hiyo jana wakati akifungua semina kwa wanachama wa taasisi ya maendeleo kwa
viziwi Tanzania (TAMAVITA) kuhusu ushiriki na uwekezaji katika masoko ya mitaji
Tanzania (CMSA).
Semina hiyo iliandaliwa
na mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA). Alisema kuwa michezo ya upatu
haramu ni kinyume cha sheria na imeharamishwa.
Mkuu huyo wa mkoa
waliwaasa wanasemina kutumia vyema elimu walioipata kama mwanga wakuelewa ni vitega
uchumi vipi vinavyopatikana katika sekta ya masoko ya mitaji.
Hivyo kuainisha njia ya
uwekezaji sahihi na zile sizizo sahihi kama vile upatu haramu, mfano dollar
jet, DECI, na mengine iliyowahi kutokea hapa nchini.
Alisema kuwa azma ya
serikali kujitoa katika umiliki na uendeshaji wa njia kuu za uchumi na kutoa
fursa kwa wananchi wake kumiliki kampuni ambazo awali zilikuwa chini ya uongozi
wa serikali.
“Kati ya hatua
zilizochukuliwa na serikali ni kuanzishwa kwa mamlaka ya masoko ya mitaji na
dhamana kama msimamizi mkuu wa mfumo wa masoko ya mitaji,” alisema Masenza.
Alisema kuwa serikali kwa kupitia vyombo vyake
kama CMSA iko makini katika kuangalia na kuhakikisha kila mtanzania anapata
fursa ya kushiriki katika mfumo wa masoko ya mitaji na pia mslahi yake
yanalindwa kwa kuzingia taratibu za kisheria na kibiashara bila kwuwepo kwa
upendeleo.
Aidha, mkuu wa mkoa huyu
aliupongeza uongozi wa mamlaka ya mitaji na dhamana kwa kuandaa na kuendesha
semina muhimu hasa ukizingatia kuwa sio wananchama wa chama cha viziwi pekee
walio na shauku ya kujifunza, bali hata wafanyabiashara, wafanyakazi,
wanataaluma na wananchi wengi bado dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji
ni ngeni kwao.
Kwa upande wake, meneja
uendelezaji wa masoko ya mitaji Tanzania, Nicodememus Mkama alisema lengo na
dhumuni ya semina hiyo ni kutoa elimu kwa taasisi ya maendeleo kwa viziwi
Tanzania ili wawe mabalozi watakaotumika kutoa elimu kwa wanachama wao.
Alisema kuwa chama cha
viziwi Tanzania kina wanachama zaidi ya milioni moja na kina matawi nchi nzima,
kwa hivyo wanasemina waliyopata elimu hiyo watatumika kama mabalozi kutoa elimu
ya dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji kwa wenzao.
Pia, alisema kuwa masoko ya mitaji yanawawezesha wawekezaji
kufaidika kwa njia nyingi kama vile kuweka akiba kwa kuiwekeza na kuongeza kuwa
kununua hisa ni kuwekeza matumizi ya baadaye.
Faida nyingine ni
kuwezesha umiliki wa makampuni kwa umma pamoja na hisa zinazoweza kuwekwa
rehani kupata mkopo.
Alisema hii ni faida
nyingine nzuri kwa wanahisa kutumia hati ya umiliki wa hisa kama rehani na
kupata mikopo katika taasisi za kifedha.
Hata hivo, Mkama alisema
kuwa hii ni semina ya pili kwa chama cha viziwi Tanzania baada ya semina dhana
ya uwekezaji katika mipango ya uwekezaji wa pamoja kwa wanachama wa taasisi ya
maendeleo ya viziwi iliyofanyika kule Songea mkoani Ruvuma mwezi huu.
Alisema kuwa licha ya
changamoto zinazowakabili za ulemavu wa kusikia kundi hili lina mwamko wa
kukamata fursa za uwekezaji katika masoko ya mitaji na kuchangia ukuaji wa pato
la kila mmoja na uchumi wa taifa kwa ujmla.
Mamlaka ya masoko ya
mitaji na dhamana (CMSA) ilianzishwa mwaka 1995 kwa sheria ya bunge namba 5 ya
masoko ya mitaji na dhamana ya mwaka 1994.
No comments:
Post a Comment