Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi akiongea na wadau mbalimbali wa mradi wa upatikanaji, matumizi na usimamizi wa rasilimali za maji katika hali endelevu wakati wa warsha iliyofanyika leo katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe, iliyoandaliwa na WWF-RWP kwa kushirikiana na Ofisi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB).
Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Sera kutoka WWF-TCO, Afisa Maji kutoka bonde la rufiji Idris Abdallah Msuya na mwenyekiti wa warsha Robert Chaula.
Lengo la mradi huu ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2016 wadau katika ngazi zote wafanye kazi pamoja katika kuleta uwiano na uendelevu wa upatikanaji, matumizi na usimamizi wa rasilimali za maji katika mto Mkuu Ruaha.

No comments:
Post a Comment