Thursday, 16 April 2015

KITABU CHA KIGWANGALLA "TANZANIA TUITAKAYO" KUSAMBAZWA NCHI NZIMA


Na Zainul Mzige wa modewjiblog

Mbunge wa Nzega ambaye amejitokeza kutangaza nia ya kugombea urais nchini ambaye pia amekuwa mtetezi mkuu wa wananchi wa jimboni kwake kupitia migodi mbalimbali Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (Mb) ameandika kitabu kiitwacho "Tanzania tunayoitaka" yakiwa ni mawazo yake binafsi ambacho anatarajia kukisambaza Tanzania nzima.

Kigwangalla katika kitabu chake amezungumzia fikra mpya za kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kutokana na urithi wa rasilimali, utamaduni na utajiri wa nguvu kazi.

“Kuna mambo misingi minane niliyoipendekeza, ambayo yakifanyiwa kazi tutapata Tanzania Tuitakayo”, amesema Kigwangalla.


"Misingi hiyo inaunda mfumo mpya wa politikoikonomi unaoitwa Ujamaa wa Kiafrika wenye Vionjo vya kibepari. Misingi imepewa jina la 'Kigwanomics.', ameongeza Kigwangalla.

Kitabu hicho cha "Tanzania tunayoitaka" kwa mujibu wa Kigwangalla mwenyewe ameeleza kuwa kinapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Iringa huku juhudi zikiendelea kusambaza Tanzania nzima.

Pata nakala ya kitabu cha Kigwangalla ambacho kipo mtaani kwako.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...