Pato la Mkoa wa Iringa limeongezeka kutoka Shilingi milioni 867,482 mwaka 2005 hadi kufikia Shilingi milioni 2,755,924 Mwaka 2013 ambapo Mkoa ulishika nafasi ya tano.
Hayo alibainika wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akitao taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa matokeo makubwa sasa (BRN) Julai, 2013 hadi kufikia Februari, 2015 kwa waandishi wa habari jana.
Alisema kuwa katika kuchangia pato la Taifa, Pato la Mkazi mwaka 2005 lilikuwa Shilingi 558,444 ambalo limeongezeka hadi kufikia Shilingi 1,660,532 mwaka 2013 na kuufanya Mkoa kushika nafasi ya pili kwa kuwa na pato kubwa la Mkazi.
“Pato la Mkoa huchangiwa kwa kiasi kikubwa na mashamba makubwa ya tumbaku, chai, viwanda vya chai, misitu na viwanda vya mbao,” alisema.
Katika sekta ya maji, alisema kuwa malengo makuu ni kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika Halmashauri zote nne kwa kujenga miradi ya maji 31 katika vijiji 42.
Aidha vituo 381 vya kutekea maji vimejengwa na 175 kati ya hivyo vinatoa huduma kwa watu 38,015.
Kwa ujumla watu wanao pata huduma ya maji safi kufikia Desemba, 2014 ni 652,278 sawa na asilimia 69.3 ya wananchi wote wa Mkoa wa Iringa.
Katika utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Miradi ya Maji ni kama ifuatavyo;
Miradi iliyokamilika ni Mradi wa pamoja wa Mawelewele, Mkoga na kitasengwa, mradi wa pamoja wa Nduli, Mgongo na Kigonzile Manispaa ya Iringa; Igangidung’u H/Wilaya ya Iringa; Kipaduka, Vitono na Ikuka H/Wilaya ya Kilolo na Igomaa, Mapanda na Kiponda H/Wilaya ya Mufindi.
Miradi iliyo zaidi ya 80% ni 10 ambayo ni: Irindi, Ihimbo, Ilamba, Ng’uruhe na Ipalamwa H/Wilaya ya Kilolo, Ikimilinzowo H/Wilaya ya Mufindi na Malinzanga, Kikombwe, Weru na Mfyome H/Wilya ya Iringa.
Miradi iliyo 60% - 80% ni 3 ambayo ni: Mwatasi na Lulanzi H/Wilaya ya Kilolo na Ukami H/Wilaya ya Mufindi.
Miradi iliyo chini ya 60% ni 3 ambayo ni: mradi wa pamoja wa Itengulinyi, Isupilo na lumuli, na miradi ya Izazi na Migoli H/Wilaya ya Iringa.
Miradi ambayo haijaanza ni 5 ambayo ni: Mosi, Ugele na Ulonge-Kigungawe, Manispaa ya Iringa, Izazi na Migoli H/Wilaya ya Iringa, Sawala-Kibao na Mkonge-Igoda H/Wilaya ya Mufindi.
Utekelezaji wa miradi kwa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa katika sekta ya afya imejikita katika huduma za mama na mtoto.
Malengo makuu ni kupunguza vifo vya mama wajawazito kutoka kiwango cha sasa cha vifo 156/100,000 (vizazi hai) hadi kufikia 150/100,000; Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kutoka kiwango cha sasa cha 9.1/1000 hadi kufikia vifo 7/1000; Kupunguza vifo vya watoto chini ya mwaka 1 kutoka kiwango cha sasa cha vifo 8.5/1000 hadi kufikia vifo 5/1000; na kupunguza vifo vya Watoto Wachanga wenye umri wa siku 28 baada ya kuzaliwa kutoka kiwango cha sasa cha vifo 8.1/1000 hadi kufikia vifo 4/1000.
Utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa
Utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa katika shughuli za afya hadi Desemba, 2014 uko kama inavyoonyesha katika viashiria vifuatavyo:
Mama wajawazito wanaozalia vituoni (wanaohudumiwa na wakunga wenye ujuzi ni asilimia 100.
Mama wajawazito wanaohudhuria kliniki katika wiki 12 ni asilimia 50. Wanawake wenye umri wa kuza (umri wa miaka 15 – 49) ni asilimia 49.
Watoto waliopatiwa chanjo ya “Pental 3” ni asilimia 94
Watoto wanaopatiwa dawa (ARV) za kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni asilimia 92
Napenda kutumia nafasi hii kutoa shukrani kwa wadau wote tunaoshirikiana katika kuboresha huduma za afya mkoani.
Aidha ninawashukuru umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu vya hapa mkoani Iringa kwa kujitokeza kutoa damu kwa wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa tarehe 11/4/2015 ambapo “units” 23 za damu zilipatikana.
Pia ninatumia nafasi hii kutoa taarifa kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa kutakuwa na wiki ya chanjo Kitaifa ambayo itaanza tarehe 24-30/4/2015.
Ninawaomba wananchi wote wa mkoa wa Iringa kuwapeleka watoto wenye umri chini ya miaka 5 kupata chanjo za kuzuia magonjwa ambazo ni muhimu sana.
Lengo la wiki hiyo ni kuhamasisha jamii umuhimu wa kupata chanjo ili kuzuia magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo ambayo ni polio, donda koo, pepo punda, kichomi, kuharisha, surua na uti wa mgongo.
“Ujumbe wa wiki ya chanjo mwaka huu, 2015 ni: “Jamii iliyochanjwa ni Jamii yenye Afya” na Kauli mbiu ni “Chanjo ni Zawadi ya Maisha.
No comments:
Post a Comment