Dereva wa gari la kampuni ya Zed's Logistics Ltd, Azizi Athumani akiwa na majereha usoni (Picha na Friday Simbaya)
Watu sita wamenusurika kifo na kukimbizwa Hosptali ya Rufaa ya mkoani wa Iringa kufuatia ajali iliyohusisha lori mbili zilizogongana uso kwa uso katika la eneo la Kibwabwa katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Mbeya mkoani Iringa.
Ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili T 939 CRE aina ya FAW lenye tenki la mafuta lenye namba za usajili T 408 CSR ambayo ni mali ya kampuni ya Pwani Haulers Ltd ya Dar es Salaam ikitokea Chunya mkoani Mbeya liligongana uso kwa uso na gari yenye namba za usajili T 361 BET aina ya DAF CF yenye tela namba T 419 BRS mali ya kampuni ya Zed's Logistics Ltd ya Dar es salaam ikielekea nchini Zambia kutoka Dar es Salaam.
Gari hilo ya mafuta likiwa limepakia mzigo wa karoti juu ya tenki la mafuta ambayo hata hivyo lilitoka kupeleka mafuta wilayani Chunya mkoani Mbeya liligongana na gari lililobeba kontena nyuma na kujeruhi watu sita waliolazwa hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Imeelezwa kuwa dereva aliyekuwa akiendesha lori lililokuwa linatoka kupakua mafuta wilayani Chunya amevunjika miguu yote miwili na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Iringa sambamba na watu wanne waliekuwepo kwenye lori hilo.
Kaini kibangali ambaye ni shuhuda wa ajali hiyo aliambia Nipashe leo kuwa ajali hiyo imetokea jana Jumapili majira ya saa 2 usiku.
Alisema kuwa ajali hiyo imetokea mita chache kutoka kwenye kibao kinachozitaka gari zitembee kwa spidi ya kilometa 50 kwa saa (50km/h) maeneo ya makazi eneo la Kibwabwa, Manispaa ya Iringa mkoani Iringa.
Naye dereva wa gari la kampuni ya Zed's Logistics Ltd, Azizi Athumani alisema alipakia mzigo ambao ulikuwa ndani ya kontena kutoka bandarini Dar kupeleka nchini Zambia, dereva huyo ni moja wa majeruhi wa ajali hiyo aliyetibiwa na kuruhusiwa kutokana na kutokuumia sana ingawa gari lake limeharibika vibaya.
Hata hivyo, Mkuu wa Usalama barabarani mkoani Iringa (RTO), ASP Leopord Fungu amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kwamba kabla ya ajali ya malori kugongana uso kwa uso, kulikuwa na ajali nyingine ya kwanza eneo hilo hilo iliyohusisha pikipiki na gari aina ya pickup.
Alisema kuwa pikipiki ilikuwa inatoka kujaza mafuta katika kituo cha afuta cha Iringa Service Station kilichopo maeneo ya Kibwabwa na kuingia barabara kuu bila kufuata sheria za barabarani na kusababisha ajali hiyo.
ASP Fungu alisema kuwa watu sita wajeruhiwa katika ajali hizo mbili na kulazwa hoapitalini ambapo wawili wameruhusiwa na wengine wanne wanaendelea na matibabu.
No comments:
Post a Comment