Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipongezwa na Mwenyekiti wa Tawi, Haji Omary Kaguke muda mfupi ya kuchukuwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani ya chama leo katika ofisi ya Mseke Kijiji cha Ugwachanya tarafa ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.
Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipongezwa na Mwenyekiti Wanawake Tawi la Ugwachanya, Elizebeth Marry baada ya katibu huyo kuchukuwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani ya chama leo katika ofisi ya Mseke Kijiji cha Ugwachanya tarafa ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.
Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipeana mikono na Mwenyekiti wa Kata ya Mseke, Imani Lucas Ngimbe muda mfupi baada ya kumkabidhi fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani katibu huyo leo katika ofisi ya Kata ya Mseke katika Kijiji cha Ugwachanya tarafa ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.
Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipongezwa na Mwenyekiti wa Jimbo la Kalenga Alex Nyulusi Kyambuke baada ya katibu huyo kuchukuwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani ya chama leo katika ofisi ya Mseke Kijiji cha Ugwachanya Kata ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.
Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipongezwa na Katibu Kata (BAVICHA) Alkhan Kalolo baada ya Menisy kuchukuwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani ya chama leo katika ofisi ya Mseke Kijiji cha Ugwachanya Kata ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.
Wakiwa ofisini
MWENYEKITI wa Jimbo la Kalenga wilayani Iringa, Mkoa wa
Iringa, Alex Nyulusi Kyambuko (Chadema) amewaomba wanachama na wananchi kwa ujumla
kuchagua viongozi watakaochochea kuleta maendeleo katika maeneo yao kipindi
hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
Alisema kuwa ili chama hicho kiweze kushinda katika Uchaguzi
Mkuu huo ni lazima wanachama wachague viongozi watakaochohea upatikanaji wa maendeleo.
Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi jana wakati wa hafla ya kumkabidhi fomu ya kuomba nafasi ya
kugombea udiwani ndani ya chama kwa Katibu Kata ya Mseke, Zolango Menisy
Mbwelwa iliyofanyika katika Kijiji cha
Ugwachanya, tarafa ya Mlolo.
Alisema kuwa watanzania wanaotaka mabadiliko na ni wakati
sasa wakujiandaa kupokea mabadiliko hayo.
Aliongeza kuwa nchi hii ina rasilimali nyingi sana lakini zinawanufaisha
watu wachache kwa sababu viongozi waliopewa mamlaka ya kuzisimamia rasilimali wameshindwa
kusimamia vizuri na matokeo yake umaskini unazidi kuongezeka.
“Tumeona pengo la walionacho na wasionacho linazidi
kuongezeka kunakopelekea wananchi wengi kukosa imani na viongozi waliopo
madarakani,” alisema mwenyekiti huyo wa jimbo.
Aliongeza kuwa chama chao kina utaratibu mzuri wa kuteua viongozi
wake ndio maana wanauhakika wakushinda Uchaguzi Mkuu mwaka huu na kushika dola
kupitia muungano wa Ukawa.
Aidha, alisema serikali watakayoiunda itahakikisha kila mwananchi
anajenga nyumba bora kutoka na vifaa vya ujenzi kushuka na ndio mwisho wa
nyumba za nyasi.
Alisema kuwa hawatarajii kuona wananchi wanaishi katika
nyumba za nyasi baada ya vifaa vya ujenzi kama vile semeti na mabati kushika
bei.
“Ili tuweze kupunguza gharama za afya kwa wananchi ni lazima
wananchi wawe na makazi bora ya kuishi,” alielezea.
Kwa upande wake, mtia nia katika nafasi ya udiwani, Zolango
Menisy Mbwelwa ambaye pia ni Katibu Kata ya Mseke, alisema kuwa endapo atabahatika
kuteuliwa na chama kupeperusha bendera katika nafasi ya udiwani na baadaye
kuchukuwa fomu Tume ya Uchaguzi (NEC), atahakikisha shule ya kata inajengwa
pamoja na zahanati.
Alisema kuwa kwa muda mrefu sasa kata hiyo haina shule ya
sekondari ya kata na wanafunzi wanatumia shule ya sekondari ya Tosamaganga kama
shule ya kata, ambayo hata hivyo iko umbali mrefu.
Kuhusu suala la zahanati, alisema kuwa kata hiyo haina kituo cha afya wala
zahanati isipokuwa wanatumia hospitali ya misheni Ipamba ambapo alielezea kuwa
huduma za afya ni kubwa kwa wananchi wa kipato cha chini.
Mwisho
No comments:
Post a Comment