Sunday, 28 June 2015

LUKUVI: MAOFISA ARDHI NDIO CHANZO CHA MIGOGORO YA ARDHI MIJINI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa wilaya ya iringa na manispaa ya iringa, kuhusiana na migogoro ya Ardhi inaokabili wananchi hao pamoja na kutowalipwa fidia ya maeneo yao. (Picha Friday Simbaya)

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kulia) akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Iringa kuhusiana na migogoro ya ardhi inaokabili wananchi pamoja na kutowalipwa fidia baada ya maeneo kupolwa. Waziri huyo alikuwa mkoani hapa ziara ya siku moja ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea masijala ya ardhi za Manispaa ya Iringa na wilaya ya Iringa. (Picha Friday Simbaya)


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) akioneshwa ramani ya mpango kabambe ya matumizi bora ya ardhi ya miaka 20 ijayo (2015-2036) na Afisa Ardhi wa Manispaa Willclif Benda (katikati) anayeshuhudia ni Mkrugenzi wa Mtendaji wa Manispaa ya Iringa Ahmed Sawa (kulia). Waziri huyo alifanya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani hapa ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea masijala za ardhi za Manispaa ya Iringa na Wilaya ya Iringa jana. (Picha Friday Simbaya)


Sehemu ya wananchi wa Manispaa ya Iringa na Wilaya ya Iringa Vijijini waliofika kumsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (hayupo pichani) kuhusiana na migogoro ya ardhi inaokabili wananchi hao jana. Waziri huyo alifanya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani hapa ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea masijala za ardhi za Manispaa ya Iringa na Wilaya ya Iringa jana. (Picha Friday Simbaya)


IRINGA: Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema asilimia kubwa ya migogoro ya ardhi mijini inasababishwa na maofisa ardhi.

Lukuvi alisema hayo alipofanya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani Iringa, ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea masijala ya ardhi za Manispaa ya Iringa na Wilaya ya Iringa jana.

Waziri huyo aliongea na viongozi mbalimbali wa mkoa na wananchi wa Manispaa ya Iringa na Wilaya ya Iringa Vijijini kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika ukumbni wa mikutano wa Siasa ni Kilimo. 

Alisema kuwa migogoro mingine ya ardhi inasababishwa kwa sehemu kubwa na maofisa ardhi na baadhi ya wananchi wakorofi kwa kushirikiana maofisa ardhi. 

Akizungumza na viongozi na wananchi wa mkoa wa Iringa, Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi alisema Wizara imepunguza kwa zaidi ya nusu gharama za upimaji ardhi kutoka 800,000/- hadi 300,000/- ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati suala ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa inatokea.

“Wizara imepunguza kwa zaidi ya nusu gharama za upimaji ardhi kutoka 800,000/- hadi 300,000/- ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati na kwa upande wa hati mliki za kimila, wizara imepunguza kodi ya ardhi kutoka 1,000/- hadi 400/- kwa ekari moja kwa mwaka kwa maeneo ya vijijini,” alisisitiza Lukuvi.


Aidha Lukuvi aliongeza kuwa sambamba na kupunguza migogoro ya ardhi, serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi na hivyo kuongeza mapato amabayo yataisiaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. 


Hata hivyo pamoja na kupunguza gharama hizo Wazrizi Lukuvi aliwaonya Maofisa ardhi, kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maafisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa linaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.


“Maafisa ardhi lazima wafanye kazi kwa kuzingatia taratibu ili kuepusha migogoro ambayo inatokea miongoni mwa wananchi na kuwasababisha kuichukia serikali yao” alisema Lukuvi.


Waziri Lukuvi alikuwa na ziara ya siku moja kwa shughuli za kikazi mkoani Iringa, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaasa viongozi wa mkoahuo kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa.

“Msitumie nguvu kubwa kutatua migogoro ya ardhi kwa sababu kwa kufanya hivyo mtaleta madhara makubwa kwa wananchi, lakini mtumie njia ya mazungumzo kutatua migogoro hiyo. Uzoefu unaonesha kwamba mahali palipotumika nguvu kubwa ya kutatua migogoro pameshindwa kuleta suluhu ya migogoro hiyo,” aliwaasa viongozi wa mkoa.



Awali, Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Wamoja alimweleza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa kwa sasa Mkoa wa Iringa una migogoro mitatu mikubwa ya ardhi.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...